Home Kimataifa Mtoto wa raisi afunga goli wakati PSG wakibeba kombe la 6 mfululizo

Mtoto wa raisi afunga goli wakati PSG wakibeba kombe la 6 mfululizo

14926
0

Timothy Weah mtoto wa raisi wa sasa wa Liberia George Weah alikuwa katika kiwango cha hali ya juu sana hii leo akiisaidia PSG kuichapa Monaco bao 4-0 na kubeba Trophees Des Champions mara 6 mfululizo.

Timothy ni mtoto wa raisi wa sasa wa Liberia George Weah lakini cha kushangaza ni kwamba Timothy yeye sio raia wa Liberia bali ni raia wa Marekani kutokana na uraia wa mama yake.

Timothy hajawahi kuicgezea Liberia hata mara moja lakini tayari ameshaichezea Marekani U-15 na U-17 na mwaka huu pia aliichezea Marekani timu ya wakubwa huku pia huh ukiwa mwaka ambao alianza kuichezea timu ya wakubwa ya PSG.

Kama haufahamu tu ni kwamba golikipa wa PSG(timu anayochezea Timothy) aliwahi kucheza zidi ya baba mzazi wa Timothy mwaka 1995 ikiwa ni miaka mitano kabla ya Timothy kuzaliwa.

Mabao mengine ya PSG hii leo yalifungwa na Angel Di Maria aliyefunga mabao mawili (32′ na 91′) na Christopher Nkunku naye akifunga bao lingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here