Home Ligi EPL Mwamuzi wa EPL atimuliwa baada ya kutukana mtandaoni

Mwamuzi wa EPL atimuliwa baada ya kutukana mtandaoni

8521
0

Bobby Madley inasemekana alituma meseji chafu kwenye mtandao wa Snapchat


Madley amefukuzwa kutumikia kama mwamuzi wa ligi kuu England (Premier League)


Taarifa zinasema kuwa kwenye ukurasa wa snapchat wa Bobby Madley ilitumwa picha ambayo iliambatanishwa na matusi.

Mwamuzi huyo mwenye miaka 32 aliachia ngazi ya kuendelea kuchezesha msimu huu kabla ya kufukuzwa kwake. Hakusema sababu zozote za msingi kwanini aliamua kusitisha huduma zake

Takwimu msimu uliopita
Mashindano M  Y  YR  R  
 Jumla 283 849 20 31
UEFA Champions League Qualifying 2 10 0 0
Europa League Qualifying 2 8 0 0
UEFA Youth League 3 16 0 1
Premier League 92 305 4 9

Mwanidishi Neil Ashton wa The Sun, alisema Madley aliweka picha ya mlemavu kwenye ukurasa wa Snapchat, huku ikiambatanishwa na maneno ya kebehi kuwa hakuna uwezekano wa kuwa na uwezo wa kushindwa mbio na mlemavu.

Shabiki mmoja alichukua picha hiyo na kuituma kwa mabosi wa chama cha waamuzi wa England.


Madley yupo kwenye zuio la kuongelea chochote popote pale kuhusiana kwanini aliondoka au kuacha kuchezesha michezo ya ligi kuu England

Kuna taarifa zinadai kuwa mwamuzi huyo yupo kwenye mipango ya kuhama nchini. Tokea ametangaza kustaafu kuna fununu kuwa anatakwenda nchini Norway.

Wasifu wake

Majina Robert Madley
Kuz 6 October 1985  (32)
Wakefield, West Yorkshire, England
Michuano ya ndani
Mwaka ligi Kaz
2013–2018 Mwamuzi
Kimataifa
Mwaka Mich Kazi
2016–18 FIFA Mwamuzi

Madley alifanya vizuri sana Premier League na alitajwa kuwa mmoja kati ya waamuzi wazuri sana Ulaya wenye weledi mkubwa. Mwaka uliopita alipitshwa na FIFA kuchezesha michezo yeyote ya kimataifa.


Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchezesha michezo mikubwa kama Manchester United vs Tottenham Hotspur na Chelsea na ule  Liverpool vs Arsenal mwezi March. Pia alichezesha fainali ya Arsenal na Chelsea msimu uliopita.

Taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa yupo kwenye mazungumzo na shirikisho la soko la Norway ambapo anataka kwenda kuchezesha.

Taarifa hizo zilithibitishwa na swahiba wake Terje Hauge alsema hayo akihojiwa na TV 2 na kusema kuwa Madley anatarajia kuchezesha Eliteserien, ligi kuu Norway.

Familia ya Maddley ilisumbuliwa sana kutoa tamko kuwa hayupo vizuri kisaikolojia baada ya kusemekana ameachana na mke wake Rachel, mwenye miaka 34, aliyedumu nae kwa miaka miwili

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here