Home Entertainment Mwana FA afanya sherehe Mourinho kutimuliwa Old Trafford

Mwana FA afanya sherehe Mourinho kutimuliwa Old Trafford

4090
0

Kama kuna watu waliokuwa wamechoka kumuona Jose Mourinho pale Old Trafford basi Mwana FA ni mmoja wao, jamaa amefurahia kusikia taarifa za kuondoka kwake, furaha yake unaweza kufikiri labda Manchester imeshinda taji  EPL!!

Mwana FA anashangaa kwa nini Mourinho amechelewa kufukuzwa licha ya kuvurunda kwa muda mrefu? Anaamini Mou alipaswa kufukuzwa kitambo na saizi watu wangekuwa wameshasahau kama alikuwa kocha wa Manchester United.

“Mimi kama mfatiliaji nadhani kuna vitu kadhaa vingeweza kufanyika lakini suala la Mourinho kuondoka lilikuwa linatakiwa kuwa la kwanza na alitakiwa aondoke muda mrefu lakini nashangaa kwa nini jamaa wamemchelewesha kiasi hicho.”

“Mbinu za modern football zimemshinda Mourinho hilo ni jambo moja lakini pia nadhani amepoteza ushawishi kwa wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.”

“Ninavyoingalia timu ina nafasi mbili au tatu za kurekebisha na akipatikana kocha mzuri inaweza kucheza vizuri sana. Kulikuwa na shida ya beki wa kulia lakini Daloti anacheza vizuri, upande wa kushoto kama Shaw hajaumia anafanya vizuri pia lakini Mou alikuwa anataka pesa ya kusajili beki wa kati lakini juna wachezaji anawaweka nje kitu ambacho hakikuingii akilini.”

“Wachezaji kama Valencia, Young, Johns, Smalling bado wanaongezewa mikataba hadi unashindwa kuelewa hawa jamaa wanaona mpira huuhuu tunaouona sisi?

“Mimi kama shabiki wa Manchester United hata ingetokea anaondoka Mourinho halafu timu anapewa Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ningekubali ilimradi aondoke tu.”

“Watu wanamtaja Zidane lakini mimi sioni kama ni mbadala hasa kwenye kitu ambacho Manchester inataka kwa sababu Madrid ya Zidane ilikuwa inacheza ‘counter attack football’ nadhani pia alikuwa anashinda kwa sababu yupo na akina Ronaldo, Bale, Modric lakini sioni mpira ambao sisi tunautaka ataweza kuucheza.”

“Kuna makocha wengi wanajua kucheza ‘modern football’, mimi ningemchagua Pochetino lakini suala la kutokuwa na kombe hata moja na lenyewe linatisha kidogo pamoja na kwamba Spurs wanacheza mpira mzuri lakini mafanikio yao makubwa ni Ericksen kumpasia Kane.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here