Home Uncategorized Mwandishi aliyevumbua skendo ya rushwa kwa raisi wa soka auawa kikatili

Mwandishi aliyevumbua skendo ya rushwa kwa raisi wa soka auawa kikatili

3483
0

Vita ya rushwa mara nyingi inahataraisha sana uhai wa waandishi endapo tu mkono wa mwanasiasa utakunjuliwa kwa maslahi binafsi.

Ghana imeingia kwenye sura mpya baada ya mauaji ya kutisha kwa mwandishi mmoja nchini humo.

Mauaji ya kikatili kwa mwandishi aliyevumbua skendo ya rushwa kwa aliyekuwa raisi wa shirikisho la soka Ghana Mh Akwesi Nyantakyo. Makala ya mwandishi huyo ilisababisha raisi wa soka nchini Ghana kufungiwa maisha.

Mwandishi huyo anayejulikana kama Ahmed Hussein-Suale aliuwawa akiwa anaendesha gari kuelekea nyumbani kwake mjini Madina-Accra. Suale alipigwa risasi ya kichwaniz shingoni na kifuani na watu waliokuwa kwenye pikipiki na wakatokomea bila kumfanya chochote. Hawakuchukua hata shilingi 10.

Hata hivyo mbunge wa Assin Central, Kennedy Agyapong amekanusha kutokuhusika na mauaji hayo ya Ahmed Hussein-Suale, na kudai kuwa alimpa onyo Suale asijaribu kuondoa mguu wake ndani ya eneo lake.

Mbunge huyo amesema mwandishi mwenzake Bwana Anas Aremeyaw ndiye anayehusika na tukio hilo baada ya kusemekana alitoa meseji za vitisho vya Suale.

Hapo awali mbunge huyo alionekana kukerwa sana na kitendo cha Mwandishi huyo kutoa taarifa hizo za kiupelelezi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here