Home Kitaifa Mwinyi Kazimoto aondoka rasmi Simba Sc, Manara ataja sababu ya kuondoka kwake

Mwinyi Kazimoto aondoka rasmi Simba Sc, Manara ataja sababu ya kuondoka kwake

18527
0

Hatimaye kiungo wa Simba Mwinyi Hassan Kazimoto amethibitisha rasmi kuacha kuitumikia klabu hiyo bingwa nchini Tanzania.

Mwanzoni kulikuwa na minong’ono ya hapa na pale kuhusu Kazimoto kutokuonekana katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi kwenye mchezo wa ngao ya Hisani na mechi dhidi ya Tanzania Prisons.

Lakini Mwinyi mwenyewe amekatisha minong’ono hiyo baada ya hii leo kupitia katika account yake ya face book kuthibitisha kuachana na Simba.

Mwinyi ameandika “Ahsante kwa mashabiki na wapenzi wa Simba kwa kipindi chote mlichokuwa na mimi, tulicheka na kulia pamoja lakini kila kitu kina mwisho.

Nashukuru kwa muda wote niliokuwa klabuni, maisha ya mpira ni safari na hii leo naanza safari yangu mpya kimpira ndani ya klabu yangu mpya, muwe na mchana mwema”.

Kazimoto kwa sasa amehamia katika klabu ya Jkt Tanzania ambao hii leo walikipiga dhidi ya KMC katika mchezo ambao uliisha mapema hii leo kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema sababu ya Kazimoto kuondoka katika klabu ya Simba ni kutokana na kuomba mwenyewe kwenda kumalizia soka lake katika klabu ya JKT.

Manara amemtakia kila la kheri Mwinyi Kazimoto katika klabu mpya aendayo na kusema Wanasimba watamiss mashuti/bunduki alizokuwa akipiga wakati akiwa Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here