Home Dauda TV Mzambia wa Lwandamina ampagawisha Manara

Mzambia wa Lwandamina ampagawisha Manara

14943
0

Ofisa habari wa Simba Maji Manara amepagawishwa na uwezo wa kiungo wao mpya Cletus Chota Chama waliyemsajili Dynamos ya Lusaka Zambia kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani.

Manara amesema, Chama ambaye pia amewahi kuichezea Zesco United anaweza kuufananisha uwezo wake na gwiji Hamis Thobias Gagalino ambaye alitamba kwenye soka la Tanzania miaka ya nyuma.

“Tumefanya usajili tumemleta mtu anaitwa Chama, ebwana sio kama namsifu lakini kwa namna nilivyomuona, hapa ana miezi sita akizidisha sana mwaka anaondoka kwenda mbele, anajua mpira hadi anakera. Huyo mtu ni balaa labda naweza kumfananisha na Gagalino, Okwi, Bocco, Kagere watakuwa wanafunga hadi wanaona tabu”-Haji Manara.

Angalia full video kupitia Dauda TV kuona Haji Manara alivyopagawishwa na mchezaji mpya wa Simba Chama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here