Home Kitaifa Mzimu wa Yanga utazamwe kwa makini

Mzimu wa Yanga utazamwe kwa makini

6816
0

Timu ya wananchi Dar es Salaam Young Africans (yanga) ni moja ya timu kongwe na kubwa hapa Tanzania, Afrika ya mashariki na kati. Misimu jadhaa hapo nyuma hasa kipindi cha kocha Hans Van De Pluijm na Chicken Man George Rwandamina chini ya uongozi wa Yusufu Manji ilikuwa yanga yenye uwezo wa kifedha, kiutendaji pamoja na iwezo mkubwa uwanjani huku wakichukua (VPL) Vodacom premier league mara tatu mfululizo mbele ya watani wao wa jadi samba pamoja na mshindani wao wa karibu Azam FC.

Mwishoni mwa msimu uliopita hasa baada ya mwenyekiti wao Yusufu Manji kupatwa na matatizo kati yake na serikkali yaliyomuweka mda mwingi kuutumia katika kutatua matatizo binafsi na ikapelekea kujitoa katika nafasi yake ya wenyekiti na club kuwa chini ya makamu mwenyekiti bwana Sanga tokea hapo yanga ilipotea na kuwa na matatizo ya kiutendaji, kiutawala na kiuchumi.

Yanga walijikuta kwenye janga kubwa la kudaiwa madeni lililopelekea kutolipa baadhi ya stahiki za wachezaji na kupelekea baadhi ya wachezaji kugoma kuitumikia timu, suala lililopelekea yanga kumaliza msimu katika nafasi nyuma ya samba na azamMsimu huu yanga chini ya kocha Mwinyi Zahela haikupewa nafasi kubwa kwenye ushindani wa kuwania ubingwa wa Tanzania bara(TPL) kutokana na uwezo wa kifedha pamoja na aina ya usajili, uwekezaji pamoja na maandalizi yao ya msimu kabla ya ligi kuanza hayakuwa na nguvu kama matokeo wanayopata.

Baada ya hayo yanga ilipitia wakati mgumu pale wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na makamu mwenyekiti kujiuzulu kwa sababu mablimbali hasa kubwa ikitokana na ukata wa kifedha ndani ya timu. Haya yote hayakuweza kukwamisha jitihada za kusaka ubingwa ambapo mpaka sasa yanga wanaongoza ligi wakicheza michezo 13 wakishinda 11 na sare mbili wakiwa na jumla ya point 35 akifatiwa na azam mwenye point 32 ambao wote kwa pamoja hawajapoteza mechi hata moja.

Pamoja na kuanza vizuri kwa yanga msimu huu lakini bado yanga ina matatizo mengi hasa kiuchumi na kiutendaji ambayo yanaweza kuathiri upatikanaji wa matokeo kadri siku zinavyoenda, ni mda mwafaka hivi sasa viongozi wa yanga na wanayanga wenyewe watafute njia sahihi ya kuyatatua matatizo yao haasa ya kiuchumi ili waweze kuwapa motisha wachezaji kuepuka matatizo ambayo yamekuwa yakitokea hasa mwisho wa msimu na kupelekea kutofanya vizuri kwa timu ikiwa wanakuwa wanaanza vizuri tatizo linakuwa kubwa kwenye kumalizia msimu kama ilivokuwa kwenye msimu uliopita, hivo ni wakati sahihi wa mzimu wa yanga kuangaliwa upya.

NAWATAKIA UCHAGUZI MWEMA YANGA NA KUFANYIA KAZI HAYA MAWAZO.
BY Raphael Lucas(Udom)
0710690782,

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here