Home Kitaifa Rais wa CAF alivyotumia jukwaa la Ndondo Cup Awards kukabidhi kijiti...

Rais wa CAF alivyotumia jukwaa la Ndondo Cup Awards kukabidhi kijiti cha AFCON

7789
0

Kati ya matukio makubwa na ya kihistoria yaliyotokea usiku wa Ndondo Cup Awards 2018 ni Rais wa chama cha soka Afrika Caf Ahmad Ahmad kukabidhi beji ya CAF kwa Rais wa chama cha soka Tanzania Wallace Karia.

Hii ilikuwa ni ishara ya Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kwa vijana chini ya miaka 17 ya AFCON inayotarajiwa kuanza May 12-29, 2019.

Ahmad Ahmad ambaye pamoja na kuisifu michuano ya Ndondo Cup 2018 ametumia jukwaa hilo la tuzo za Ndondo kuirasmisha Tanzania katika michuano ya AFCON U17.

AFCON U17 2019 itakuwa ni mara ya 13 kwa CAF kuandaa michuano hiyo ambayo itakuwa na washiriki 8 huku timu ya vijana Tanzania Serwngeti Boys tayari wameshafuzu moja kwa moja kutokana na uenyeji wao katika michuano hiyo.

Mwezi May mwaka 2015 ndio Tanzania ilitangazwa kuandaa michuano hii ambapo timu nne za juu katika michuano hii wataliwakilisha bara la Afrika kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa U17 nchini Peru.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here