Home Ligi Kuu Bara Nani anaiyumbisha Singida United?

Nani anaiyumbisha Singida United?

8991
0

Kuna wakati mambo hayakai. Yaani hayaendi kabisa. Sio kwa sababu tu huna uwezo ila inatokea tu.Singida United wamesajili wachezaji 14. Bila shaka hiyo ni timu mpya sasa. Wakati timu kama Alliance wakitegemea vijana wao. Singida bado wanahisi wanahitaji majina mapya.Tatizo la Singida kwa haraka haraka ni dogo tu. Waswahili tunasema usioe kabla hujajipanga. Singida walisajili wachezaji wakubwa na kuwaahidi maslahi makubwa na mwisho wa siku wamekwama. Malengo yao yakikiwa makubwa kuliko mipango yao. Kitendo cha kushindwana na Pluijm ni kigezo tosha kuwa mengi yalikuwa kwenye maandishi kuliko utekelezaji (Nawaza tu)Kila mchezaji waliyemtegemea ameondoka. Kutinyu, Kaseke na hata yule musdhathiri tuliyesikia Azam wamezozana leo hayupo.Unajiuliza kwanini uondoke Singida wakati palionekana pana neema? Au wadau wakubaliane na mimi kuwa sio kila king’aacho ni dhahabu. Inawezekana Singida ni gari la Lakshari lilikokuwa likiendeshwa ovyo. Haiwezekani unapangua timu nzima wanabaki wachezaji wanne! Haipo hiyo. Imetokea Singida tu. Yaani walifanya kama zile timu zinazopandaga daraja huku zikiwa hazina hela na mwelekeo. Timu hizo mara nyingi ndo zinakuwa na msemo kwamba “Kila mtu asepe na chake”Wamempoteza mwalimu Pluijm. Tena wakasema aliwahujumu. Mbaya zaidi ameondoka na wachezaji muhimu. Timu imeanza upya. Imetoka mjini inarudi kijijini kuanza maisha upya. Mwisho wa siku msimu ujao akina Kyombo watamendewa tena na Simba na Yanga nao wataondoka.Mimi nina amini lengo la Singida ni jema kabisa wala hawana matarajio mabaya. Lakini wajiulize waliyumba wapi. Kuna wakati kweli maisha tu yanakataa. Ushawahi kuona Messi na Ronaldo wanabaki na goli wanakosa unajiuliza imekuwaje?Msimu huu michezo mitatu ya awali wameambulia alama 4. Wamepigwa na Biashara ndani ya Namfua, kabla kuwaadhibu Mwadui na kutoka Sare tasa na Mbao Fc.Msimi uliopita katika michezo yake mitatu ya awali walifungwa ugenini na Mwadui bao 2-1, Kabla ya kutoa kichapo kwa Mbao Fc na Stand United.Sio kwamba Singida wameanza vibaya sana lakini ni kwa namna walivyoshindwa kufurukuta katik uwanja wao wa nyumbani katika michezo yao miwili inaonesha dalili mbaya.Inawezekana hapo baadae timu ikakaa sawa lakini sina imani kama ile Singida tuliyotarajia ituwakilishe kimataifa itafanikiwa katika nyanja hiyo. Tumeona mmoja ya mdhamini wake ameachana na klabu hiyo. Siku sio nyingi hawa nao tutasikia hali ya uchumi sio njema. Kwa sababu mwekezaji anapokuja kwako na asione matunda atakimbia.Wanapaswa wakae chini wajue wanakosea wapi ili wajirekebishe. Singida ina nguvu kubwa na ni timu iliyotabiriwa mema.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here