Home Ndondo Cup Ndondo Cup 2018 imetisha na imetuachia somo hili

Ndondo Cup 2018 imetisha na imetuachia somo hili

10581
0

Ndondo Cup ina shangwe la kibabe.

Ukiondoa baadhi ya mechi kubwa za Simba na Yanga au Azam na Singida hakuna mechi zinazovutia zaidi kuzidi ndondo Cup. Balaa la Manzese na Kivule utadhani ni Simba na Yanga.

Mashabiki wana upendo wa dhati na vilabu vyao. Watu hawashabikii hizi timu kwa kuwa wanazijua, ila ile spiriti ya timu kutoka eneo lao. Kuhusu Ndondo kufunika hata VPL sio maneno yangu bali ni Maneno ya Anko Mrisho Ngassa.

Ndondo imebeba uhalisia

Ugumu wa viwanja, uchumi wa kati, mazingira magumu ya utendaji kazi hizzi ni safia halisi za soka la Afrika. Ndondo imebeba maana halisi ya soka letu na utamaduni wetu. Kucheza kwenye uwanja mbovu haya ndiyo mazingira ya Afrika. Ndondo inapaswa iwe hivyo. Maneno ya Edo Kumwembe

Ndondo ni kioo

Mpira wa ndondo ni mgumu sana. Baadhi ya wachezaji hujifunzia ndondo ili kuweza kuhimili mikikimikiki mbalimbali. Ramadhan Kabwili anakiri kuwa wachezaji wa ndondo wanatoa picha halisi ya mchezaji wa ligi kuu anapaswa kupambana vipi.

Ndondo inalinda utamaduni

Kuna vigoma, kuna machifu wanaowakikisha vilabu vyao, kuna vitimbi vya kila aina ambavyo vinaelezea maisha ya tamaduni mbalimbali, Jana tumetumbuizwa na sholomwamba aliyekuwa akisimamia sana upande wa Singeli. Yote haya yanaleta pamoja ila ladha halisi ya utamaduni wetu maisha yetu ya mtaani, na sana mbalimbali.

Ndondo inaunganisha watu mbalimbali

Tumeona watu wa Beko kuna mabalozi kutoka afrika kusini, tumepata Mcheza ina mabalozi kutoka Kenya. Je huoni kama ni fursa mbalimbali kwa washika dau? Na wao pia wataenda kututangaza huko kwao. Hii yote ni kwa sababu ya Ndondo Cup.

Ndondo inatoa fursa

Tumeona baadhi ya akina mama wakisifia namna biashara zao zinaenda vizuri na wakitamani ndondo iendelee tena na tena. Watu wengi wanapata manufaa ya kiuchumi kupitia michuano hii.

Ndondo inavuta mpaka hisia za viongozi

Juzi kati Kangi Lugonga alialikwa kwenye nusu fainali ya Ndondo Cup. Hata mh Rais aliwahi kuzungumzia Ndondo Cup. Fainali imepata bahati ya kuhudhuria na watu wakubwa sana nchini hapa. Kumbe hata viongozi wakubwa nao wanavutiwana michuano hii kwa kiasi kikubwa.

Meya wa ubongo, mkuu wa mkoa, waziri wa zamani bwana Mwiguli, naibu waziri wa michezo, viongozi wa vilabu mbalimbali, raisi wa TFF na wengineo wengi leo walikiwepo hata viongozi wa simba. Wapo wasanii tuliowaona siku ya ufunguzi kama akina Aslay, Madee nae leo alikuwepo, akina Nikki wa pili yaani Ndondo Cup imehudhuriwa na watu mashuhuri (Wanyama, Samatta na Abdi Banda)

Kwenye Ndondo kuna aman ni Usalama

Unajua kuna watu ukiwaambia neno NDONDO katika akili yao wanawaza kuna vurugu ubabe, n.k. Michuano ya Ndondo hakuna hayo mambo. Mashabiki ni watulivu. Ni sehemu sahihi kabisa. Kuna watu wanadhani refa wa ndondo anachezesha akiwa na panga kiunoni.

La hasha hata moja ya marefa hodari kabisa wanaotambulika na FIFa Sasi akikuwepo. Hakukuwa na vurugu wala utakatishaji wa aina yeyote wa matokeo.

Ndondo Cup ni mchezo wenye ushindani mkubwa

Tumeona fainali ya leo. Ushindi kiduchu kabisa. Inaonesha wazi kuwa mambo sio lelemama. Fainali kadhaa zilizopita mshindi alipatikana kwa matuta. Washindani wamekuwa na uchu wa kurudisha furaha kwa mashabiki wao.

Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here