Home Kitaifa Ndondo Cup mchangani hadi FIFA

Ndondo Cup mchangani hadi FIFA

10720
0

Kama una kumbukumbu nzuri utakuwa unakumbuka fainali ya kwanza ya #SportsXtraNdondoCup2014 pale kwenye uwanja wa Bandari, Tandika.

Fainali hiyo iliwakutanisha waliokuwa mabingwa wa kwanza Abajalo FC dhidi ya Tabata United waliofungwa kwa penati huku penati ya mwisho ikifungwa na Kelvin Sabato maarufu kama Kiduku ambaye kwa sasa anachezea Mtibwa Sukari ya Morogoro inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara lakini wakati huo baada tu ya mashindano alijiunga na Mwadui FC ikiwa ligi daraja la kwanza na kuisaidia kupanda ligi kuu huku yeye akiibuka mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza.

Nataka kukukumbusha kuhusu waliosimamia mchezo huo, kwa maana ya waamuzi, kama una kumbukumbu nzuri katikati alisimama Hery Sasii akisaidiwa na Helen Mduma pamoja na Idd Lila wakati Shafii Mohamed yeye alikuwa fourth official.

Waamuzi hawa wakati huo walikuwa katika kiwango cha kawaida tofauti na ilivyo sasa ambapo watatu kati yao wanatambuliwa na Fifa ambao ni Hery Sasii, Helen Mduma pamoja na Idd Lila.

Haya ni mafanikio makubwa kwa #NdondoCup kuona watu waliopita kwenye mashindano haya wanafanikiwa na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Hery Sasii aliyesimama katikati katika fainali hiyo amekuwa mwamuzi bora wa ligi kuu Tanzania bara kwa misimu miwili mfululizo sasa na hii ni kutokana na kazi yake nzuri anayoifanya pindi anaposimamia dakika 90 za mchezo.

Kesho Jumapili August 5, 2018 fainali ya 5 na #NdondoCup itachezwa katika uwanja uliotumika kwa fainali ya kwanza lakini mwaka huu zikibadilika timu pekee ambapo Manzese United itakabiliana na Kivule United.

Cha kufurahisha zaidi nachukua fursa hii kuwatambulisha tena waamuzi walewale waliochezesha fainali ya kwanza ndio watakaochezesha fainali ya 5.

Mwamuzi kijana mwenye kujiamini Hery Sasii atasimama katikati akisaidiwa na Idd Lila pamoja na Helen Mduma, hawa wote wanatambuliwa na Fifa huku mezani akiwa ni Shafii Mohamed.

Hii ni historia ya aina yake na ya kupendeza kwenye michuano ya #NdondoCup2018.
#MstueMwana na mwana amstue mwana fainali ya #NdondoCup Jumapili kwenye uwanja wa Bandari, Tandika. Milango itakuwa wazi kuanzia saa 5:00 asubuhi kwa kiingilio cha shilingi 3,000 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here