Home Kitaifa Ndondo Cup yazidi kufungua njia kwa vijana, safari hii ni kipa wa...

Ndondo Cup yazidi kufungua njia kwa vijana, safari hii ni kipa wa Mlalakuwa Rangers

8579
0

Michuano ya Ndondo Cup imeendelea kuwa fursa kwa wachezaji baada ya golikipa Haruna Mandanda kusajiliwa na timu ya Mbeya City.

Mandanda aliyekuwa anaichezea Mlalakuwa Rangers ameeleza jinsi michuano hiyo ilivyomsaidia hadi sasa hivi anacheza ligi kuu Tanzania bara.

“Michuano ya Ndondo Cup ni mizuri, sasa hivi inapata nafasi na sehemu nyingine za Tanzania, kijana yoyote anayepata nafasi ya kucheza ukifanya vizuri utaenda sehemu nyingine.”

“Nawapa hamasa vijana wenzangu, wakifanya mazoezi na kupata nafasi ya kucheza Ndondo Cup naamini watafikia malengo yao.”

“Nikiwa Mlalakuwa Rangers msimu huu tulianzia hatua ya makundi tukaenda 16 bora tukafika robo fainali tukatolewa na Goms United.”

“Mara ya kwanza kabisa nilipofatwa na viongozi wa Mbeya City wakitaka kunisajili, nikijisikia faraja kubwa sana kwa sababu ilikuwa ni ndoto yangu kucheza ligi kuu.”

“Kila kitu ni malengo na unapokuwa na malengo katika jambo fulani utafikia malengo, watu wengine wanaichukulia poa Ndondo Cup wanawaza kucheza wapate pesa lakini Ndondo Cup ni kama daraja la kukufikisha sehemu nyingine kwa sababu inaangaliwa na watu wengi wakiwemo viongozi wa ligi kuu na ligi nyingine.”

“Nimesaini miaka mitatu Mbeya City, ndio naanza kucheza mpira watu wengi hawanifahamu kwa hiyo nahitaji muda mrefu wa kucheza kuliko maslahi. Watu wanaweza kuona miaka mitatu ni mingi sana inaweza kuwa michache kwangu kwa kutafuta kitu ninachokitaka.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here