Home Ligi BUNDESLIGA Nguzo tegemezi za Mourinho, Klopp na Pep Gurdiola zimeanguka ,wataweza peke yao?

Nguzo tegemezi za Mourinho, Klopp na Pep Gurdiola zimeanguka ,wataweza peke yao?

16420
0

Kesho mchezo wa ngao ya hisani unapigwa kati ya Chelsea vs Manchester City. Hii ni kama honi/kiashirio cha msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu wa 2018/2019 kuanza.

Kuna mambo mengi mapya watu wanatamani kuona, ikiwemo kocha mpya wa Chelsea Marizio Sarri namna ambavyo anaweza kuirudisha Chelsea katika chati.

Juegen Klopp, Jose Mourinho na Pep Gurdiola wenyewe wapo tu kama wapinzani waliopita ,japokuwa msimu huu unaoanza wote watakuwa na mapigo makubwa.

Wote hawa watatu baada ya kipindi kirefu sana watacheza msimu wao wa kwanza bila wasaidizi wao ambao wamekuwa nao kwa muda zaidi ya miaka 10 katika mabenchi yao.

Pep Gurdiola na Domenec Torrent. Pep na Torrent walianza kufanya kazi pamoja mwaka 2007 tangu wakiwa Barcelona B na baadae kwa pamoja wakapanda hadi Barcelona timu ya wakubwa.

Pep na Torrent walikwenda wote Bayern Munich kabla ya kuja Man City lakini mwaka huu mwezi uliopita Torrent alibwaga manyanga kuwa msaidizi wa Pep Gurdiola.

Torrent kwa sasa ni kocha mkuu wa New York City Fc huku Mikel Arteta akirithi mikoba yake kwa Gurdiola, Torrent pamoja na Pep wametwaa makombe 24 tangu wakiwa Barcelona B.

Jurgen Klopp na Zeljko Buvac. Hawa nao wamekaa kwa miaka 17 pamoja, Klopp na Buvac walikutana tangu kabla ya Borussia Dortmund walianza kufanya kazi Mainz mwaka 2001 ndio baadae wakaenda BVB.

2008 hadi 2015 walikuwa pamoja Borussia Dortmund na safari yao kwenda Liverpool ilikuwa moja, mwezi April Buvac aliacha usaidizi wa Klopp japo bado ni muajiriwa wa Liverpool.

Bado kwenye website ya Liverpool Buvac anaonekana kama moja ya makocha wa Liverpool na labda upo uwezekano wa kurejea katika benchi la ufundi la Liverpool katika msimu ujao wa ligi.

Jose Mourinho na Rui Faria. Hawa ndio ambao wamekuwa gumzo kubwa kwa sasa na wengi wanataka kuona je Faria ndio alikuwa anamshauri Mou kuhusu basi au kupaki basi ilikuwa ni style ya Jose Mourinho.

Faria na Mou nao walikutana mwaka 2001 wakapiga kazi Porto baadae Chelsea, kisha wakenda Inter Milan, wakaenda Real Madrid, wakarudi Chelsea kabla ya kuhamia Manchester United.

Tangu Faria aiache Manchester United hali imekuwa si hali, Jose amekuwa akilalamika kila kukicha huku msimu mpya wa ligi bado hata haujaaanza lakini madhara ya Faria yameanza kuonekana.

Inasemekana kwamba kati ya vitu ambavyo Mourinho alikuwa akivuna kwa Faria ilikuwa namna ya kuwapa moyo wachezaji kupambana na hii inaweza labda ikaanza kuwa shida mpya United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here