Home Kimataifa Ni Manchester United dhidi ya Arsenal

Ni Manchester United dhidi ya Arsenal

5602
0

Mchezo wa ligi kuu England, Manchester United, atakuwa nyumbani katika dimba la Old Trafford, kumkaribisha Arsenal, mchezo huu umeibua maswali mengi kutokana na historia za hizi timu miaka ya nyuma pia na hata msimu huu miendelezo yao.

Hakuna mtu asiyejua kuwa Manchester United, ana rekodi nzuri mbele ya Arsenal, ikumbukwe mara ya mwisho Arsenal, kumfunga Manchester United, katika dimba la Old Trafford, mnamo mwaka 2006 goli lilofungwa na Emanuel Adebayor, je? imedumu miaka mingapi tangu Arsenal, apate ushindi katika uwanja wa Old Trafford, miaka 12 sasa umepita hiyo ni nilikuwa historia fupi kiujumla

.
Katika mchezo wa soka historia ina nafasi yake na tunahiheshimu kama tunavoelewa lakini Arsenal, ya msimu huu ipo vizuri kwa maana ya kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji wana wachezaji waliokamiliki wanaocheza mpira mzuri wanajituma tunaona kabisa Emery, amefanya mapinduzi katika ligi kuu ndo kwanza ana msimu moja tu. .
.
Ukiangalia katika msimamo wa ligi kuu England mpaka sasa Arsenal, wapo nafasi ya nne wana alama 30 na wamefunga mabao 30 na wameruhusu mabao 18 ukitoa idadi ya mabao ya kushinda na kufungwa wanabakia na mabao 14 ukiangalia Arsenal, katika safu ya ushambuliaji wapo vizuri zaidi kwenye ufungaji ila katika swala la safu ya ulinzi aipo vizuri sana ipo wastani kuelekea mchezo huu naiona Arsenal, itakuwa bora katika idara hiyo kuliko Manchester United.
.
.
Manchester United, wapo nafasi ya nane wana alam 22 wamefunga mabao 22 na wamefungwa mabao 23 tunaiona Utd, ambayo aipo vizuri kwenye idara ya ulinzi mpaka safu ya ushambuliaji kuelekea mchezo huu naiona Manchester United, inaenda kupata tabu kuwakabili Arsenal. .
.

Jose Mourinho, ni kocha ambaye ana uwezo mkubwa wa kuzicheza mechi ngumu kama hizi kwa maana ya kutumia mpira mirefu pale wanapopata mpira ukiangalia Arsenal, wachezaji wao wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi me naamini Jose, muda mwingi timu yake itakuwa inacheza chini kwa maana ya kujilinda zaidi. .
.
Arsenal, wana asilimia kubwa ya kutawala mchezo kila sehemu wana wachezaji wazuri wenye ubora, huu mchezo Arsenal, wataweza kuamua matokeo kwenye safu yao ya ushambuliaji.

@tunuhassan57

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here