Home Kimataifa Ni Mauro Icard na Lorenze Insigne, Seria A hapatoshi leo

Ni Mauro Icard na Lorenze Insigne, Seria A hapatoshi leo

3985
0

Leo Inter wanawakaribisha Napoli ndani ya uwanja wao wa Meazza mjaira ya saa 3 usiku.

Inter imeshindwa kabisa kupata bao dhidi ya Napoli kwa dakika 406 mara ya mwsio ilikuwa mabao ya Marcelo Brozovic April 2016 in a 2-0. Internazionale wameshinda mechi 2 tu dhidi ya Napoli ndani ya Serie A (D3 L2). Inter wameshinda mechi 2 kati ya 6 walizocheza Serie A msimu huu (D2 L2), baada ya kushinda mechi 7 mfululizo.

Mtukutu Radja Nainggolan hatakuwepo katika mchezo wa leo. Radja alipigwa marufuku na Inter kutokana na utovu wa nidhamu.

21 May: alistaafu baada kukatwa Ubelgiji🇧🇪
14 July: Ubelgiji wakamaliza nafasi ya 3 🥉
20 Dec: akadai kuwa amelaghaiwa €150k 💰
20 Dec: Ikasemekana amewaambia marafiki zake anataka kurudi Roma
23 Dec: Akasimamishwa na Inter 🇮🇹
Huu ulikuwa mwaka wa matatizo kwa Radja

11/03/18, 20:45 Inter – Napoli 0 : 0
21/10/17, 20:45 Napoli – Inter 0 : 0
30/04/17, 20:45 Inter – Napoli 0 : 1
02/12/16, 20:45 Napoli – Inter 3 : 0
16/04/16, 20:45 Inter – Napoli 2 : 0
30/11/15, 21:00 Napoli – Inter 2 : 1
08/03/15, 20:45 Napoli – Inter 2 : 2
19/10/14, 20:45 Inter – Napoli 2 : 2
26/04/14, 20:45 Inter – Napoli 0 : 0
15/12/13, 20:45 Napoli – Inter 4 : 2

Inter wameshinda mechi zote 6 za mwisho walizocheza nyumbani na kuzuia nyavu zao kutokuguswa mechi 5 kati ya hizo 6. Mara ya mwisho Nerazzurri kucheza mechi 6 mfululizo bila kuruhusu bao ilikuwa April 2010.

SSC Napoli wamepata alama 41 baada ya michezo 17 huku wakiwa alama moja nyuma ya alama walizopata msimu wa 2017/18 alama (42).

Mara ya mwisho Napoli kupata sare ugenini ndani ya Serie A ilikuwa katika uwanja Meazza dhidi ya AC Milan: Baada ya hapo wameshinda mechi 8 na kufungwa 3.

Takwimu za Napoli

Nyumbani Ugenini
5 Ushindi 4 1
9 Kupoteza 2 7
8 Sare 3 5

Takwimu za Inter

Nyumbani Ugenini
9 Ushindi 7 2
5 Vipigo 1 4
8 Sare 3 5

San Siro ndio uwanja ambao fowadi wa Napoli Dries Mertens amecheza zaidi ya mara mbili na kushindwa kufunga bao: Amecheza mechi 10 (5 vs Inter na 5 vs AC Milan).

Raisi wa Napoli  Aurelio De Laurentiis amesema hana imani na mwamuzi Paolo Mazzoleni.

Huyu mwamuzi ana upendeleo wa wazi kabisa kila anapochezesha mechi zetu. Sina imani nae hata kidogo”

Mchezo wa leo utavutia sana na baadhi ya nyota wa vilabu hivi kama Icard na Insigne watatupia jicho la tatu kutokana na uwezo wao. Hata hivyo Lorenzo Insigne amefunga bao 1 tu Serie A dhidi ya Inter katika michezo 11 moja ya rekodi mbaya kwa timu ambazo amewahi kucheza nazo mechi nyingi na kufunga idadi ndogo ya magoli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here