Home Ligi EPL Ni Vita ya mafundi Maurcio Pochettino vs Jurgen Klopp, Kane vs Salah,...

Ni Vita ya mafundi Maurcio Pochettino vs Jurgen Klopp, Kane vs Salah, moto unaendelea kuwaka DSTV

45130
0

Baada ya UEFA Nations League, hauna haja ya kurudisha rimoti kwani DSTV Moto hauzimi na unaendelea kuwaka wikiendi hii kwa ligi mbali mbali kuendelea kupigwa.

Jumamosi hii macho ya wapenda soka wengi yatakuwa Wembley ambapo Tottenham Hotspur watakuwa wakiwakaribisha Liverpool katika muendelezo wa ligi ya EPL, mchezo ambao DSTV watakuonesha moja kwa moja mapemaa kutokea pale Wembley.

Liverpool huwa hawaachi kutoka na walau bao moja wakikutana na Tottenham, mara ya mwisho kwa Klopp kushindwa kupenyeza mpira kwenye lango la Tot ilikuwa ni kwenye mechi yake ya kwanza zidi ya Tottenham mwaka 2015.

Hadi sasa rekodi ambayo Tottenham wanashikilia ya alama nyingi ni alama 12 baada ya michezo 15 na kama wataifunga Liverpool Jumamosi hii baasi watakuwa wameifikia.

Lakini Liverpool wenyewe wanatafuta kushinda mechi yao ya 5 mfululizo msimu huu, hii sio mara ya kwanza kwao kufanya hivi kwani 1978/1979 walifanya hivi lakini pia 1990/1991 walifanya hivi pia.

Ukichukua na mchezo wao wa mwisho msimu uliopita, Liverpool wameshinda mechi 5 zao za mwisho EPL na kama watashinda mechi ya kesho baasi itakuwa ya 6 mfululizo na hii ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014.

Katika michezo 9 ya nyumbani(EPL) ya Tottenham wameshinda michezo 8 huku mchezo pekee ambao walipoteza ilikuwa zidi ya Man City, mechi ambayo walifungwa 2-1 mwezi April.

Pamoja na kufunga sana lakini Harry Kane hajawahi kufunga katika mechi 5 mfululizo za Tottenham nyumbani, kama akiifunga Liverpool ataingia kwenye kundi la Jermain Defoe na Son Heung Min ambao ni nyota pekee kuwahi kufanya hivyo.

Wembley sio mahala pazuri kwa Liverpool kwani tangu baada ya kuifunga Everton 2-1 kwenye nusu fainali ya FA mwaka 2012 hawajawahi kupata ushindi katika mechi zao zote 4 zilizofuatia Wembley.

Na kwa taarifa yako tu ni kwamba ukiacha mechi kati ya Everton na Arsenal(151), mchezo kati ya Liverpool na Tottenham unafuatia kwa kuwa na idadi nyingi ya mabao 149 katika EPL.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here