Home Kimataifa Nina mawazo tofauti na Shaffih Dauda kuhusu sakata la mchezaji bora wa...

Nina mawazo tofauti na Shaffih Dauda kuhusu sakata la mchezaji bora wa dunia

14049
1

Sakata la kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa dunia limegeuka kuwa hoja nzito.


“Shaffih Dauda anaamini kuwa Leo Messi pamoja na Griezmann walistahili. Kwa mtazamo wangu mimi napingana na hoja zake alizoainisha. Mwanzoni Dauda alisema Salah anastahili Ballon d’Or leo haamini kama Salah anapaswa kuwepo tatu bora, inaonekana kombe la dunia limebadilisha msimamo wake”

Griezmann anasema: “2016 nilipoteza fainali mbili na nikamaliza watatu kwenye Ballon d’Or nyuma ya Messi na  Ronaldo mwaka huu nimeshinda fainali tatu nilipaswa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu bora” 

Griezmann anaona hajatendewa haki hata. Kilio chake ni kwamba  FIFA wamemnyima wasaa wakuingia kwenye listi ya wachezaji watatu bora.

Kuna vigezo watu wanatumia kuwa bingwa wa dubia lazima aingie kwenye orodha hiyo. Sio sheria kwamba ni lazima lakini kweli imewahi kutokea mara kadhaa orodha ya wachezaji bora zikachukuliwa na timu zilizocheza fainali za kombe la dunia.

Mwaka 2002  orodha ya wachezaji watatu wote waliingia fainali [Brazil Vs German]

1 BrazilRonaldo
SpainReal Madrid 169
2nd Brazil Roberto Carlos Spain Real Madrid 145
3rd Germany Oliver Kahn Germany Bayern Munich 110

2006 [Ufaransa Vs Italia]

1 ItalyFabio Cannavaro
SpainReal Madrid 173
2 Italy Gianluigi Buffon Italy Juventus 124
3 France Thierry Henry England Arsenal 121

Tuzo hizo zilishirikisha wachezaji waliofika fainali pekee yake. Lakini sio sheria. Wala hatuishi kwa mazoea.

Mshambuliaji huyu wa Atletico Madrid alikuwa mchezaji bora wa tatu kwenye fainali za kombe la dunia nyuma ya Luka Modric na Eden Hazard kule nchini Russia 2018. Na siamini kama alikuwa kivutio kikubwa kwenye kombe la dunia.


Sawa alifunga mabao 23 kwa Atletico Madrid katika michezo 33 na kutwaa ubingwa wa Europa League pamoja European Super Cup.

“Ni jambo la aibu na la kushangaza” Alisema Griezmann.

“Hii tuzo si inatolewa na FIFA, Si ndio? Tumeshinda kombe la dunia lakini hakuna mmoja wetu [Mfaransa] katika tuzo zao. Ni uamuzi wao lakini wametushangaza.


Mbali na mitazamo ya wengi akiwemo  Shaffih Dauda, mimi bado naamini Salah, Modric na Ronaldo walistahili kwa asilimia zote kuwepo.


Tujiulize  nini maana ya mchezaji bora? Je mchezaji bora ni yule mwenye mafanikio mengi au yule aliyefanya makubwa na kuvutia watu kumtazama?


Nimesoma barua ya FIFA ya mwaka 2016.

Hii Hapa. Inaelezea mchezaji bora ni nani?

Ukiisoma vizuri barua hiyo inatanabaisha kuwa mchezaji bora atachaguliwa kwa sifa zifuatazo

  • Kuonesha kiwango kizuri uwanjani
  • Na kuwa mfano wa kuigwa nje na ndani ya uwanja.

Hakuna mahali FIFA wameainisha kuwa mchezaji bora anapaswa kubeba makombe yapi. Ila imeeleza tu kiufupi kwamba unapaswa kuonesha kiwango ambacho kitaleta uzito wa aina yake kwa jamii kiasi cha kuwavutia wengine na kujizolewa jina kubwa miongoni mwa watazamaji.

Soka ni mchezo wa furaha. Unachopaswa kufanya mchezaji ni kuwa balozi wa soka unapokuwa uwanjani na nje ya uwanja. Watu wanataka burudani. Hivyo FIFA wanapokupa tuzo wanakushuruku kwa kuwa balozi wao.

“Kuna watu watakataa”

Watu wanasema Messi alistahili. Kama ni suala la kipaji sawa nakubaliana nao. Messi ana kipaji kuzidi mchezaji yeyote aliyepo uwanjani, lakini mwisho wa siku mpira ni mchezo wa watu wote.

Messi alikuwa na msimu mzuri sana ndani ya La Liga, lakini  FIFA na La Liga ni bodi mbili tofauti.

Messi ni mchezaji bora wa La Liga bila shaka. Huenda alifanya vizuri UEFA kwa kiwango kikubwa lakini je Messi anawazidi Salah na Ronaldo kwenye UEFA? Sizungumzii mafanikio ya makombe nazungumzia uwezo binafsi walioonesha. Wala hakuna haja ya kuliongelea sana. Salah na Ronaldo wana mafanikio UEFA kumzidi Messi.

Salah alikuwa mchezaji bora wa EPL kila tuzo alibeba na aliweka rekodi zake. Hakuishia hapo hata UEFA nako alifanya makubwa akiwa na klabu ambayo wengi waliidhania kuwa dhaifu. Huyu ni mchezaji bora wa Afrika lakini watu hawaoni hilo. Mchezaji bora ni yule anayevutia wengi kwa wakati huo kutokana na kuwaburudisha wengi. Bila Shaka msimu uliopita hakuna ambaye hakumsikia Salah. Sio ndani ya uwanja pekee hata mambo aliyofanya nje ya uwanja. Tena suala la nje ya uwanja Salah aliteka hisia za wengi na alikuwa mfano wa kuigwa na alisimama hasa kama balozi wa soka.

Hatuwezi kumfananisha Modric na Varane au Griezmann kutokana na majukumu ya uwanjani lakini tunaweza kuwafananisha kwa namna walivyoibuka kuwa mashujaa wa timu zao. Varane ni mmoja wawachezaji bora wa Madrid lakini shujaa wa Madrid Ramos alimtosa kwenye beki bora wa Madrid kwenye michuano ya UEFA. Varane alikuwa mmoja wa nyota wa Ufaransa na pia alikuwa mchezaji tegemezi. Lakini ayari Mbappe na Kante walionekana kuwa mashaujaa na wachezaji hatari zaidi. Varane alifaa kuingia lakini tuzo ilikuwa inahitaji wachezaji watatu tu. Na ilikuwa ngumu kwake kuingia kwenye orodha hiyo.


Messi alifeli na Argentine, akafeli na Barcelona UEFA.


Modric aliibeba Croatia ambayo hakuna aliyeamini hata kama ingefuzu hatua ya 16 bora, alisimama kidete na kutwaa tuzo wa kiungo bora wa UEFA na bila shaka alikuwa kiungo bora wa La liga. Hakuishia hapo tu alitoa burudani la kipekee mbele ya watu bilioni 4 duniani waliokuwa wakifuatilia kombe la dunia. Hakika alistahili tuzo hiyo bora ya dunia.


Je Griezmann amtoe nani?

Griezmann hakuna alichowazidi Modric wala Ronaldo wala Salah kwa kigezo cha mafanikio binafsi ya kijumla. Hatuangalii klabu imekufanyia nini ila tunaangalia umeifanyia nini klabu. Griezmann hakuwa na Takwimu zozote bora kuwazidi Ronaldo, wala Salah hata Messi hakumzidi chochote. Griezmann kwangu hakuwa nyota wa Ufaransa, bali namuona Kante na Mbappe. Mbappe ndiye mchezaji aliyehofiwa zaidi ufaransa. Maana yake Mbappe ndiye nyota wa Ufaransa.

Tuangalie data zake za kwenye ngazi ya klabu msimu wa 17/18
GRIEZMANN  M  G  Y YR   D
Jumla 49 29 15 8 1 3.872′
32 19 9 7 1 2.530′
8 6 4 630′
6 2 2 1 529′
3 2 183′

Inawezekana Griezmann alipaswa kuingia kwenye tuzo hii lakini je UEFA alifanya vizuri? Jibu hapana. Griezmann alikuwa mshambuliaji lazima tumpime kwa mabao. Mashindano yote ambayo ameshindana na aidha Messi au Ronaldo au Salah hajawazidi chochote ispokuwa tu kombe la dunia ambalo bado mimi nasisitiza hakuwa nyota au mchezaji hatari wa timu ila (Mbappe)

Tumwangalie Ronaldo ambaye alikuwa na mafanikio ya upande mmoja zaidi.

RONALDO  M  G  A  Y YR   D
Jumla 44 44 8 3 1 3.678′
27 26 5 1 2.297′
13 15 3 2 1.170′
2 2 180′
1 7′
1 1 1 24′

Griezmann kwa ngazi ya vilabu alicheza dakika 3872 ana mabao 29, alicheza zaidi ya dakika 200 zaidi ya Ronaldo aliyecheza 3.678 huku akifunga mabao 44. Je Griezmann angestahili mbele ya Ronaldo? Amecheza dakika 200 zaidi ya Ronaldo lakini bado Ronaldo alimzidi mabao 15. Tena akiwa na mgawanyiko mzuri sana wa mabao hao, La Liga 26 kwenye mechi 27, na Uefa 15 kwenye mechi 13. Maana yake Ronaldo alikuwa na mgawanyiko mzuri wa mashindano mawili tofauti, ngazi ya ligi na klabu bingwa.

Kwa Upande wa Salah data zake za msimu wa  17/18

Mo Salah  M  G  Y  YR  D
Jumla 52 44 16 1 4.119′
36 32 11 1 2.920′
13 10 5 929′
2 1 180′
1 1 90′
Namba hazidanganyi. Griezmann ana mabao 29 Salah ana mabao 44. Salah alihusika kwa mabao 60 ikiwa ni pamoja na kutengeneza mabao 16. Griezmann ukijumlisha asisti zake na mabao yake hiyo ni idadi ya mabao ya kufunga pekee ya Mo Salah yaani mabao 44. Shaffih dauda anataka kuniambia tukiweka makombe pembeni nikamuomba apange orodha ya washambuliaji bora Griezmann angewazidi haya? Kama mafanikio binafsi Ronaldo na Salah wamemzidi Griezmann hakuwa bora kuwazidi ila timu Ufaransa ilikuwa bora kuliko Misri na Ureno hilo ndio jibu sahihi ambalo tunaweza kumjibu Griezmann.
Timu inapobeba makombe bado sio tiketi ya mchezaji kuwa bora. Misri ilikuwa timu mbovu kuliko Ufaransa ndio maana Griezmann yupo kwenye timu iliyopata mafanikio. Watu wanataka kudharau soka la Afrika. Jitihada za Mo Salah ziliivusha Misri mdomoni mwa DRC akiwa na mabao tano. Misri ikarudi tena kombe la dunia kwa mara nyingine tokea mwaka 1994.
Sitaki kuongelea sana takwimu za Messi za msimu uliopita. Kama alivyosema Felipe Luiz kweli Messi ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee kwa kizazi hiki. Kwangu mimi pia ndiye mchezaji hatari zaidi duniani kwa kipindi chote nilichowahi kuangalia soka.
Lakini narudia tena, soka ni mchezo wa watu wote. Tuzo sio suala la klasi ila ni fomu. Messi ana klasi kubwa kuliko Salah lakini Salah alikuwa kwenye fomu sawa na ya Messi tu. Tena alimzidi Messi fomu ya UEFA. Kwa Mantiki kwamba tukihesabu magoli ya Salah hadi hatua ya Robo fainali ya UEFA ambapo Barcelona ilitoka bado Messi alizidiwa magoli na Salah.
Lakini pia nimkumbushe Shaffih Dauda baada ya mchezo wa Liverpool dhidi ya Roma alisema Salah ndiye mchezaji bora wa Ballon d’Or. Wakati anatamka hayo alijua wazi kuwa mbele kuna kombe la dunia na aliamini kombe la dunia halitabadilisha chochote lakini leo anamtoa Salah.

Mwisho niseme wachezaji wote mliowataja walistahili kuingia kwenye tatu bora lakini hata hao waliotajwa walikuwa na msimu mzuri hata kama hawakubeba makombe hayo. Hamuwezi kuniambia Mario Gotze ni bora kuliko Messi eti kisa Messi hajawahi kubeba kombe la dunia. Ubora wa mchezaji sio makombe ila ni jitihada zake na burudani.


Makala na Privaldinho (Instagram)


Usiache kutufuatilia kwenye Dauda Tv (Youtube) kujua kila kinachoendea nchini Uganda kwenye mchezo wa kimataifa. Usiache kupitia Instagram, twitter na facebook kwenye account zote za Shaffih Dauda kupata habari Kemkem.

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here