Home Kimataifa Nini kinachomtesa Henry?

Nini kinachomtesa Henry?

4498
0

Thierry Henry hili ni jina maarufu sana katika ulimwengu wa soka la sasa. Vijana wengi sana wanaopiga soka Uingereza wana mtaja sana kama mmoja kati ya watu aliowahamasisha katika soka la ushindani akiwemo mchezaji wa sasa wa Man United Paul Pogba.

Miezi kadhaa iliyopita Henry alitangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Monaco baada ya timu hiyo kua na mwanzo mbaya wa msimu. Kabla ya kupewa timu Henry alikua kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Belgium akimsaidia Martinez kma kocha mkuu walifanikiwa kufika hatua kubwa WC kwa kumaliza kama mshindi wa 3.


Henry yule mchezaji yawezekana sio huyu Henry wa ukocha.

Mechi 14
—————-
Ushindi mechi 3
———————————–
Sare mechi 2
———————————–
Vipigo mechi 9
———————————–
Nafasi ya 19
———————————–
Alama 34 kumfikia PSG
———————————–
Alama 2 kutoka mkiani


Wakati anapata shavu la kuenda kukinoa kikosi hicho cha Monaco alitabiriwa makubwa ambayo nazani kama aliyasoma ndiyo yamemfanya leo anafungwa na timu inayoshika mkia huko Ufararansa (Guingamp).

Jana Monaco wamefungwa na Guingamp uwanja wao wa nyumbanii . Na katika historia za timu hizo ni kuwa Guingamp hajawai kushinda uwanja wa Monaco (Louis ll) . Jana wameweza kuvunja mwiko mbele ya Henry.


Klabu ya Monaco inawinda saini ya kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas kwenye dirisha dogo ili kuokoa jahazi hilo – taarifa na Daily Mail


Mpaka sasa Monaco inashika nafasi ya pili kutoka mkianii maombi yanatakiwa sana kwa Henri kwa wapenda soka wote maana huyuu ni kipenzi cha wengii . Tumuombee asije akajiwekea rekodi mbaya ya kushusha timu daraja na wakati ngazi ya uchezaji alikua ni Gwijii wa maGoli.

Uwanja wa nyumbani kwake ndo imekua kma machinjio yake mwenyewee .amecheza mechi 9 kati ya hizo kafungwa sita. Hii sio rekodi nzuri kwake na kunifanya nijiulize maswali.

Ujumbe kutoka kwa Edger Edson


Shaffih Dauda kwa sasa anapatikana katika ukurasa wake mpya wa Instagram ujukikanao kama Shaffih Dauda baada ya ule wa awali kudukuliwa


MATUKIO KATIKA PICHA

Shabiki wa Wolveshampton akimkabidhi kocha wa klabu hiyo Nuno zawadi ya Krismas


Taarifa pia zinadai kocha mpya wa United Ole Gunnar anawinda wino wa mshambuliaji aliyekuwa klabuni hapo Joshua King kwa kitita cha £25

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here