Home Kimataifa Novak Djokovic ashinda Us Open 2018 na kuweka Grand Slam 14 kabatini

Novak Djokovic ashinda Us Open 2018 na kuweka Grand Slam 14 kabatini

7008
0

Baada ya mwanadada kutoka Japan Naomi Osaka kushinda taji la Us Open kwa upande wa wanawake hapo jana, asubuhi ya leo Mserbia Novak Djkovic ameshinda taji hilo kwa upande wa wanaume.

Djokovic ameshinda taji hili baada ya kumchapa Juan Martin Del Potro kwa seti 6-3 7-6 6-3 na shii inakuwa Grand Slam yake ya 14.

Uzoefu ulionekana kumbeba Djokovic hii leo kwani mpinzani wake hii ilikuwa fainali yake ya kwanza ya Grand Slam kucheza tangia ashinde michuano ya Us Open mwaka 2009.

Grand Slam 14 pia za Djokovic zimemfanya kuwa na idadi sawa ya Grand Slams na Mmarekani Pete Sampras huku vinara wa tuzo hiyo wakiwa Rodger Federer(20) akifuatiwa na Rafael Nadal(17) na kisha Djokovick

Novac alibeba Australian Open 2008, 2011, 2012, 2013, 2015 na 2016 akabeba French Open mwaka 2016, Wimbledon 2011, 2014, 2015 na 2018 kisha Us Open mwaka 2011, 2015 na 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here