Home Kimataifa Nyota hawa vibarua vyao vimebuma

Nyota hawa vibarua vyao vimebuma

4538
0
Kuna baadhi ya wachezaji kwa sasa hawana mikatabakutokana na sababu mbalimbali. Ifuatayo ni orodha ya nyota ambao wanahaha ulaya kwa sasa bila mikataba

# 1 Vincent Enyeama – kipa – 36 Miaka
Akiwa na  LOSC mkataba wake uliisha mwezi June. Mnaijeria huyu kwa sasa hana mkataba na timu yeyote na taarifa za ndani ziandai kuwa anajiandaa kustaafu soka.


# 2 Glen Johnson – Beki wa kulia – 34 miaka

Baada ya miaka 12 ya  Premier League akiwa na Portsmouth, Chelsea, Liverpool, na Stoke City, kwa sasa hana klabu ni mchezaji huru


# 3 Pepe – beki wa kati – 35 miaka

Alikuwa mmoja kati ya wachezaji walioisaidia Ureno kutwaa ubingwa wa Ulaya 2016. Hivi majuzi amevunja mkataba wake na Besiktas. Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa licha ya kwamba ni mtukutu.

# 4 Papy Djilobodji – beki wa kati – 30 miaka
Aliporudi kutoka kwa mkopo Dijon, msenegal huyu alikataa kuendelea na Sunderland, ambayo ilishuka daraja hivyo akaamua kuvunja mkataba wake.


# 5 Florentin Pogba – Beki wa kushoto-28 miaka

Baada ya mgogoro na wachezaji wenzake ndani ya klabu ya Genclerbirligi, amejikuta akizururua hapa mjini bila klabu. Ndugu yake huyu na Paul Pogba wa Man United pia aliwahi kuichezea klabu ya Saint-Etienne. Ingawa kuna taarifa kuwa anafanya mazoezi ndani ya klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary.


# 6 Didier Ndong – Kiungo mkabaji- 24 miaka

Raia huyu wa Gabon bado umri wake n mdogo hivyo ana wasaa wa kupata klabu nyingine.


 

# 7 Yaya Touré – Kiungo – 35 miaka
Amehudumu klabuni hapi miezi 4 tu na  Olympiakos, na amehusishwa na kurudi EPL kwenye klabu ya  Crystal Palace.


# 8 Alberto Aquilani – kiungo – 34 miaka

Amevitumikia vilabu vya Pescara, Las Palmas, Sassuolo na Sporting Lisbon.amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi na hali hiyo imefanya kukosa klabu mpaka sasa. Anaamini bado soka linamhitaji licha ya kuwa na umri mkubwa.


gettyimages

# 9 Préjuce Nakoulma – winga Wing – 31 miaka

Baada ya kuitumikia sana  FC Nantes raia huyu wa Burkinabe kwa sasa hana klabu huku akitajwa sana kujiunga na vilabu vya Uturuki


Dennis Grombkowski / Bongarts / Getty Images

# 10 Lacina Traoré – fowadi – 28 miaka

Hajafikisha miaka 30 lakini Monaco imevunja mkataba wake baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.


# 11 Samir Nasri – winga wa kushoto – 31 miaka
Baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Uturuki kwa sasa yupo West Ham akifanya majaribio huku taarifa zikidai atajiunga na wagonga nyundo hao wa London.


# 12 benchi

Geoffrey Jourdren, Jesus Gamez, Serdar Tasci, Yann Jouffre, Florian Martin, Mauricio Pinilla, Giuseppe Rossi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here