Home Uncategorized Nyota wa Liverpool hajalipwa miezi minne

Nyota wa Liverpool hajalipwa miezi minne

2863
0

Tumekuwa na kasheshe kubwa sana katika ligi kuu bara kuhusiana na mishahara. Vilabu vingi Tanzania vinalalamikiwa kwa tabia ya kushindwa kutoa huduma stahiki za wachezaji wake.

Sio bongo tu hata huko kwa wenzetu nako matatizo kama haya nayo yanajitokeza. Inawezekana vyanzo vya shida hii vikawa tofauti. Kwa hapa kwetu shida kubwa ni ukata lakini kwa wenzetu sababu ni tofauti.

“Nimewapa siku 10 wanilipe hela yangu kufikia sasa sijapewa chochote. Nimeshapeleka malalamiko FIFA”

Hayo ni maneno kutoka kwa swahiba wa karibu na Kipa wa Liverpool Karius anayekipiga kunako klabu ya Besikats kwa mkopo.

Jarida moja la Ujerumani limefukua siri nzito kuhusiana na fukufuku la malipo la Karius. Fununu zinadai kuwa Karius anadai mshahara wa miezi minne.

Karius amekuwa akilaumiwa sana na mashabiki pamoja na uongozi kwa ujumla kwa kiwango kibovu.

Ni kocha Senol Gunes ambaye hajaficha hisia zake na kusema waziwazi kuwa Karius anazingua.


“Mechi yetu dhidi ya Kanyaspoor magoli yote mawili ni uzembe wake. Ana kipaji lakini ana matatizo binafsi. Hajitumi na hana ushirikiano mzuri na wenzake.”

Hapo awali raisi wa klabu hiyo aliwahakikishia kuwa atambakiza Karius klabuni hapo lakini tayari uvumi huu wa mkataba unachafua mwelekeo.

Sio mara ya kwanza sakata la Karius na klabu hii kuhusu mkataba wake kufukuta. Hapo awali iliwahid kudaiwa kuwa mkopo wake utasitishwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here