Home Kitaifa Okwi huyoo ‘Sauz’, rasmi Chama kuvaa ufalme

Okwi huyoo ‘Sauz’, rasmi Chama kuvaa ufalme

9367
0

Mshambuliaji wa Simba Emauel Okwi anakaribia kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na tayari Okwi ameshakubaliana masuala binafsi na klabu hiyo.

Inaelezwa ofa ya Kaizer Chiefs kwa Okwi ni nzuri (dau la usajili na mshahara) hata yeye ameshindwa kuipiga chini na kuamua kuomba aruhusiwe kuondoka Simba akajiunge na miamba hiyo ya Afrika Kusini.

Okwi amebakiza miezi 6 kwenye mkataba wake na Simba, kumzuia  kujiunga na Chiefs kwa sasa ni kumuandalia njia ya kuondoka bure baada ya mkataba wake kumalizika.

Simba na Chiefs wamekubaliana kila kitu ila bado kuna vitu vichache havijakamilika kwa asilimia 100, kwa sasa  Simba wamefika hatua ya makundi wataruhusiwa kuongeza wachezaji na kupunguza wengine ambao Okwi atakuwa mmoja wa watakaoruhusiwa kuondoka baada ya kupata mbadala wake.

Kaizer Chiefs ni miongoni mwa vilabu vikubwa vya Afrika Kusini ambayo itampa Okwi fursa ya kucheza Soweto Derby pamoja na vilabu vingine vikubwa vya ligi hiyo kama Mamelodi Sundowns.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here