Home Kitaifa Pamba SC kuikabili Kagera Sugar CCM kirumba

Pamba SC kuikabili Kagera Sugar CCM kirumba

7950
0

Klabu ya Pamba Fc leo watashuka dimba la CCM Kirumba kupambana na Klabu inayoshiriki ligi kuu bara Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Mexime.

Pamba Fc ambao ni Mabingwa mara moja ligi kuu Tanzania mwaka 1990 na mabingwa mara mbili wa Nyerere Cup ambapo kwa sasa linajulikana kama Azam Federetion Cup mwaka 1989 na 1992 watashuka dimba leo muda wa saa 10 katika dimba hilo kwa kiingilio cha 2000 tu.


Maendeleo ya soka kanda ya ziwa?


Msemaji wa chama cha Soka mkoa wa Mwanza amesema sasa hamasa ya soka kanda ya ziwa na Mwanza kwa ujumla imeongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya mwenendo wake kudidimia. Kwa sasa ni vilabu viwili inayowakilisha jiji la Mwanza nayo ni Alliance Football Club na Mbao FC.

Kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa imetoa na vilabu takribani 6 kishiriki ligi kuu.

Biashara, Alliance, Mbao, Mwadui, Stand United na Kagera Sugar.

Klabu ya Mbao imefanikiwa kwa kiasi kupambana kubaki ligi kuu ili kulinda heshima ya jiji la Mwanza ambayo haoo awali iliwekwa na Pamba SC kwa kushiriki ligi kuu misimu mingi.


Mwenendo wa soka Mwanza na ushindani kwa ujumla?


Hata hivyo kumekuwa na ushindani mkubwa wa Mbao Fc dhidi ya Pamba. Ikumbukwe mwezi Septemba 3 mwaka 2017 Pamba SC ilicheza na Mbao fc katika mchezo wa kirafiki uliosakatwa Uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba.

Mtanange huo kumalizika kwa Pamba kuinyuka Mbao FC kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0, goli lililotiwa kimyani na Meshack Kibona baada ya mchezaji wa Mbao kumchezea madhambi mshambuliaji wa Pamba kwenye eneo la penati na mwamuzi kuawazadia Pamba tuta.


Pamba SC wamejipanga vipi?


Pamba SC ilimsajili kocha wa Zamani wa JKT Oljoro Juma Yusuph Khamis ili kuhakikisha timu hiyo inarudi ligi kuu bara. Hata hivyo msemaji wa klabu hiyo Johnson James hakutanabaisha kuwa kandarasi ya mkufunzi hiyo ni ya muda gani.

Klabu pia iliweka wazi kuwa Khamis atasaidiwa na Kocha wa Makipa wa Pamba sc, Khalfan Mbonde ambao wote wamekuwa wakifanya jitihada za kurudisha heshima ya klabu hiyo.

Klabu hiyo pia itapata huduma za kitaalamu kutoka kwa mwanandinga wao wa Zamani Yangoo Mamboleo ambaye ameteuliwa kuwa meneja mkuu wa klabu hiyo.


Pamba wanajivunia nini kwenye historia yao?


Pamba SC ni moja ya klabu pekee kutoka jiji la Mwanza kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara na kutwaa mataji mawili ya FA.


Jitihada zao zipoje?


Jitihada zao za kujaribu kupata ubingwa wa Nyerere Cup/ASFC kwa mara nyingine zilikatishwa mnamo Mwezi januari mwaka 2018 baada kupata kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu wa kutoka mji wa Shinyanga Stand United na kutupwa nje ya mashindano hayo na ndoto zao kuzima.

Mabao ya Tariq Seif dakika 24, Ndikumana Landay dakika 51 yalihitimisha ndoto ya klabu hiyo.


Harakati zao za kurejea ligi kuu?


Msimu uliopita Pamba SC wanaoshiriki ligi daraja la kwanza walikuwepo kwenye timu 32 ambazo zilifuzu kwenda hatua ya mchujo wa ligi kuu wakiwa kundi C pamoja na vilabu vya Alliance, Oljoro, Biashara, Transit Camp, Dodoma FC, Toto na Rhino.

Pamba FC walimaliza watano katika kundi hilo wakiwa na alama 15 na juhudi zao kuzama ndani ya ziwa Viktoria.


Naitwa Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here