Home Kimataifa Pata madini kuelekea Copa del Rey El Clasico 2019

Pata madini kuelekea Copa del Rey El Clasico 2019

3470
0

Barcelona Vs Real Madrid

Barcelona wanajiandaa kuwakaribisha Real Madrid kwenye uwanja wa Camp Nou, kwenye mechi ya nusu Fainali ya kwanza ya Copa del Rey.

……Barcelona walicheza kwa kiwango kizuri kwenye mechi iliyopita dhidi ya Sevilla, ambapo walishinda 6-1. Lakin wanamkosa mchezaji muhimu kwenye safu ya ulinzi Samuel Umtiti. Rafinha anakosekana pia.

……Messi na Dembele hawako fiti sana kuivaa Real Madrid, ila kulingana na umuhimu wa mechi yenyewe, tunaweza kumuona Messi akicheza hata kama hatakuwa fiti sana.

……Madrid walifungwa 5-1 na Barcelona, na Messi hakuwepo. Madrid wamerudi kwenye kiwango chao. Wameshinda mechi 5 mfululizo na wamefunga magoli 16 kwenye mechi hizo.


……Benzema pia amerudi kwenye kiwango chake pia baada ya kuanza msimu kwa kusuasua. Nategemea mechi itaamuliwa eneo la kiungo pamoja na pembeni ya uwanja.

……Kukosekana kwa Umtiti, kunamfanya kocha Valvede awapange Gerard Pique na Lenglet. Ila atajiuliza maswali ni beki yupi wa pembeni kati ya Nelson Semedo na Sergio Rorbeto atakayeweza kuendana na kasi ya Marcelo?

……Bila shaka ni Semedo nafikiri, maana ni bora kwenye kuzuia kuliko Roberto ambaye licha ya kucheza vizuri mechi zilizopita, bado kuzuia sio mzuri kama Semedo.

……Barcelona wana mapungufu kwenye kuzuia mipira ya hewani au( Set pieces) Hivyo, Madrid watalazimika kutumia udhaifu huo ili kuwaadhibu huku wakitegemea kuanzisha mashambulizi kupitia kwa Marcelo

……Lakini Marcelon ni hatari sana kwenye kushambulia kupitia pembeni ya uwanja.
Kitakachowapa faida Barcelona uwepo wa Messi uwanjani.

……Rakitic, Busquet na Arthur Melo, watakuwa kwenye idara ya kiungo ili kuiongezea timu uimara pia kuhakikisha Coutinho, Suarez na Messi au Malcom wanapata huduma.

……Kwa upande wa Madrid, wana mabeki wazuri wa kati na warefu. Sergio Ramos na Raphael Varane. Kwa mipira ya hewani hawana shida sana ukilingakisha Lenglet pamoja na Pique.

……Madrid, bila shaka watapanga viungo wa siku zote, Modric, Casemiro na Kroos. Endapo Messi akianza itakuwa changamoto nyingine kwa Casemiro.


……Hakuna kazi ngumu sana kama kumdhibiti Messi dakika zote 90 bila shida yoyote. Messi akishambulia Rakitic atakuwa anarudi kuziba nafasi yake ili asiruhusu Gareth Bale na Marcelo waanzishe mashulizi ya kushitukiza.

……Uwepo wa Dan Calvajal utasaidia kuendana na kasi ya Jordi Alba wa Barcelona. Mechi ya mapema ya Laliga ambayo Barcelona walishinda 5-1

……Nacho alicheza upande wa beki wa kulia, niliona jinsi alivyoshindwa kupambana na Jordi Alba. Bale amekuwa mvivu kurudi kuzuia.

……Atapaswa kuwa makini kwenye kushambulia na kurusi kumsadia Marcelo ili kuepuka kuepuka kuwapa nafasi Barcelona kuanza kushambulia.

Makala na Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here