Home Ligi EPL Pata yaliyojiri mkutano wa Chelsea kuelekea mchezo wao dhidi ya Newcastle

Pata yaliyojiri mkutano wa Chelsea kuelekea mchezo wao dhidi ya Newcastle

8097
0
Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amefanya mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo kuelekea kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza wakati Chelsea itakaposafiri kumenyana dhidi ya Newcastle United siku ya jumapili ya tarehe 26-Agosti.
Hapa nakuletea baadhi ya mambo aliyoyazungumza kwenye mkutano wake huo alioufanya kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham Training Centre.
Alipoulizwa kuhusu wachezaji kuuelewa mfumo wake, kocha alijibu na akisema anaamini wachezaji wake wanajitambua na wanaelewa hivyo haitokuwa ngumu kwao kuelewa jinsi ya mfumo ulivyo.
IMG_20180824_151732
Alipoulizwa kuhusu Eden Hazard na Ruben Loftus-Cheek kubaki, kocha alisema kwamba ana imani Hazard hatoondoka klabuni hapo lakini pia akasema kwa upande wa Loftus-Cheek alizungumza mara mbili katika wiki hii na anaona nyota huyo ataendelea kubaki Chelsea.
Alipoulizwa kuhusu kumuanzisha Hazard kwenye mchezo dhidi ya Newcastle united, kocha Sarri alijibu akisema “Kwangu naamini bado hajawa sawa kucheza kwa dakika zote tisini. Nafikiri anafaa zaidi kucheza kwa dakika 50 au 60. Lakini mwenyewe anataka kucheza kwa dakika zote ingawa siamini kama ni wakati sahihi kwake kucheza kwa dakika zote tisini”
Alipoulizwa kuhusu Mateo Kovacic kucheza kwenye mchezo huo, kocha Sarri alisema “Yeye pamoja na Hazard walicheza vizuri kwenye dakika 30 za mchezo uliopita dhidi ya Arsenal. Lakini sifikiri kama atakuwa sawa kucheza kwa dakika zote tisini labda kwa dakika 50 au 60,”
IMG-20180818-WA0077
Alipoulizwa kuhusu mfumo wa ukabaji unaotumika Chelsea kama ataweza kutumia malinzi watano, kocha Sarri alisema “Hapana. Sifikirii kutumia mfumo huo, niliwai kuutumia hapo kabla lakini sio kwasasa”
Alipoulizwa kuhusu mchezo dhidi ya Newcastle na anamzungumziaje kocha wa klabu hiyo, Rafa Benitez, kocha Sarri alijibu na kusema “Kwanza niseme asante kwake. Alinisaidia sana maana kabla sijafika Napoli aliitengeneza timu vizuri na kunifanya nisipate kazi sana kuingizia mfumo wangu. Nadhani ni kocha mzuri”
inCollage_20180820_195935658
“Lakini pia kuhusu mchezo unaofata, nafikiri ni mchezo mgumu kwetu haswa kutokana na ubora wa kocha na ugumu wa klabu yenyewe. Chelsea ilipoteza dhidi yao msimu uliopita, kwa hiyo nautazama kama mchezo mgumu sana kwetu”
Kocha Maurizio Sarri ataiongoza Chelsea katika mchezo wake wa tatu wa ligi kuu Uingereza jumapili hiyo ya tarehe 26-Agosti ikicheza dhidi ya Newcastle united na itahitaji ushindi ili ifikishe alama 9 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
NEWCHE

taarifa na Barnabasi kutoka darajani 1905

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here