Home Kimataifa Paul Pogba ndani ya miwani mpya

Paul Pogba ndani ya miwani mpya

6340
0

Goli nane, alama sita ndani ya mechi mbili chini ya kocha Ole Gunnar Soskjaer, ndani ya kipindi kifupi Manchester united wameonekana kuwa bora sana kiuchezaji hata kimbinu.

Wachezaji wameonekana kuhamasika sana na ule umoja uliowekwa mizizi ya chuma ndani ya viunga vya Old Trafford na Sir Alex ferguson umeonekana kuanza kuchipua tena.

Hii ni baada ya Manchester united kuonekana kupoteza dira chini ya mreno Jose Mourinho, lakini jibu la swali la nini kimebadilika ndani ya timu na olle gunnar solkjaer ameongeza nini ndani ya timu.

Jibu ni rahisi sana alichokifanya kocha huyo ni kuongea na roho za wachezaji kuliko akili zao ,kwa kuwaminisha kuwa wao wanastahili kuwa ndani ya jezi za mashetani wekundu.

Kilichobaki kwao ni kutumia jasho lao hata damu zao kwa ajili tu ya ushindi ndani ndani ya timu, kwa kila dakika zilizopo mbele yao katika roho ya pobga amerejesha mapenzi kwa timu kama yale ya Romeo na Juliet.

Namna Pogba anavyotawanya mipira kwa akili kubwa anaanza taratibu kufananishwa na mtambo uliofungwa ndani ya tanesco wa kusambaza umeme [power distributor ].

Huku macho yake yakionekana kupata miwani sahihi ambayo imemfanya mpaka sasa awe na goli mbili ndani ya mechi mbili.

Hachezi karibu tena na eneo lake la ulinzi mda mwingi kama alivyokuwa chini ya Mourinho jambo linalompa nafasi ya yeye kutumia vizuri kile kilichomo ndani ya miguu yake. Kwa macho ya mbali Manchester united chini ya Olle Gunnar Soslkjaer inaweza kuwa salama zaidi kuliko ile iliyokuwa chini ya mourinho kwa taswira fupi iliyoonekana ndani ya michezo miwili.

Kocha kwa sasa anachokifanya ni kuwaonyesha wachezaji sanamu ya ferguson na mikanda ya kile walichokuwa wakikifanya wao enzi za kina Ryan Giggs, Eric Cantona baada ya wachezaji kuishi kipindi cha kupewa mzigo wa lawama na kocha mourinho

Muda ndo ufunguo sahihi wa yale yaliyofungwa mbele ya kuta zaa bongo zetu kitu pekee ni kusubiri kama Olle Gunnar atafanikisha kuyarudisha maisha ya maziwa na asali amabayo kwa mechi walau amejaribu kuyaonesha ,tusubiri tuone.

Ujumbe kutoka kwa Meshack Malele

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here