Home Kimataifa Perreira amgomea Lukaku

Perreira amgomea Lukaku

11707
0
Lukaku ameshindwa kumshawishi kinda wa Man United Pereira kuchezea timu ya taifa ya Belgium na hatimaye ameamua kwenda Brazil

Andreas Pereira alisema mshambuliaji wa Manchester United alimshwishi mara kadha. Romelu Lukaku alijitahidi kumshawishi Pereira mwenye miaka 22, aliyezaliwa nchini Belgium.

Alichagua kuichezea Brazil U-20 ambapo baba yake Pereira bwana Marcos, ambapo alizaliwa kabla ya kwenda kuishi maisha yake Belgium ambapo alicheza soka lake la kulipwa.

Pereira pia alichezea Brazil U-23 na atacheza michezo ya kirafiki kati yao na United States na El Salvador.

“Lukaku alinifuata akaniambia kuwa nicheze Belgium. Kwangu mimi kuna utofauti mkubwa wa kucheza Brazil na kucheza Belgium.

“Lukaku akaniambia nisikilize kile kinachotoka moyoni mwangu.”

“Niligundua nafasi yangu ipo Brazil ila kimwili nipo Belgium. Wakati tunafungwa baoa 2-1 na Belgium wakati ule nilikuwa nchini Belgium lakini nilijikuta nimekumbwa na huzuni”

“Kila mmoja alikuwa akishangalia mwisho wa siku ikabidi nitoke kwenye chumba walichokuwa wakiiangalia mpira maana sikuweza kuendelea kuangalia”

“Baada ya mchezo baba alinifuata na marafiki zake wakaniambia nirudi Brazil tu maana nafsi yangu ipo upande huo”

Alisema Perreira.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here