Home Ligi EPL Pochettino atokwa na povu kuhusu United, kila mtu apambane na hali yake

Pochettino atokwa na povu kuhusu United, kila mtu apambane na hali yake

11003
0

Pochettino alimpanga muasi wa mkataba Toby Alderweireld kwenye kikosi kilichopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Fulham. Toblby anakimbia mihogo baada ya kusikia harufu ya pilau kwa jirani. Haoni chochote pale Tott. Anataka kwenda Man United klabu kubwa duniani. Hata ingekuwa ni wewe unatumia baiskeli unapewa gari huwezi kususa.

Jose Mourinho bado hajakata tamaa kwa kijana huyu kwa sababu tayari Toby amekwisha toa ulimi akionesha wazi udenda unamtoka. Tayari anapapatika na na hana furaha tena Tott. Mchezaji wa aina hiyo kwenye timu ni sumu kwenye chakula hasa kwa wenye njaa kama Tott.

Huenda mahari ya Alderweireld ikapelekwa January wakati Tottenham itakapolazimika kumtoa kabla hajaondoka bure.

Pochettino ameshtua wengi sana. Na hili ni wazi kuwa ametoa baraka kwa yeyote anayetaka kwenda kwemye ndoa nyingine. Amesema yupo tayati kutoa talaka kwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka amechoshwa na makelele kuwa wachezaji wake hawana furaha.

“huu utakuwa mwisho wa mimi kuongelea mambo yale yale,” alisema Pochettino, alipoulizwa kuhusu Alderweireld kama atabaki klabu hapo kwa misimu mingine zaidi Tottenham

“siwezi kuongelea tena suala hili maana ni mambo ya mtu binafsi. Nitaongelea kile mnachokiona uwanjani kuhusu masuala ya wachezaji binafsi hiyo sio kazo yangu”

“nimeshakwambia wachezaji wanaweza kubaki na kuondoka pia, nataka mchezaji ajitoe kwa moyo wake wote, mchezaji ambaye hana furaha basi anaweza tu kwenda hakuna tatizo, pia kuna uwezakano pia wakabaki kama wataongea na Daniel [Levy, Mwenyekiti wa Tottenham] hilo pia lipo nje ya uwezo wangu.

“Ninamhitaji mchezaji ambaye yupo na utayari wa kupambana. Wachezaji waliopo hapa nachojua wapo tayari. Hakuna aliyenifuata na kuomba suluhisho lolote au kuniambia ana shida. Nashangaa kuona watu wanaongea sana. Sawa ni mawazo yao”

“kitu pekee cha uhakika na cha ukweli ninachoweza kuwaambia mashabiki wa Tott ni ule unaonihusu mimi pekee yangu. Leo nipo tayari kumsikiliza kila mchezaji kile anachohitaji. Wakikaa basi wajitume, lakini sitarajii kesho kusikia mtu analalamika kuwa mimi ni mkali sana. Nimetoa nafasi mtu aje aseme anachokihitaji’.

“Binafsi inachosha sana. Kama kuna wachezaji au mchezaji hana furaha najua ni kawaida hiyo maana hakuna mchezaji anapenda kucheza na sio kukaa benchi.

“Nyie mmeweka sheria wachezaji wawepo 11 uwanjani, kwanini hazikusema wachezaji wawepo 22 au 24 au tuwe kama mpira wa kikapu kila mchezaji abadilike mara kwa mara? Nimechoka niacheni nifurahie soka.

“Nipo hapa kama mkufunzi kwa sababu bodi imenichagua na sijachagulia kwa sababu mimi ni mzuri wa sura. Labda pia yawezekana uzuri wa sura yangu unachangia (akacheka) Hapana! Kila siku nipo hapa napoteza muda mwingi sana kujaribu kupambana na changamoto kubwa mbele yetu. Najua mpira umebadilika umekuwa biashara na kila mtu analinda maslahi yake kila mtu anafanya hiki kile na ……….. duh duh duh, daa daa, doo doo too.

“Nasema hivi, siwezi kupoteza muda wangu kuongelea hali za watu, kila mtu apambane na hali yake” kama wanavyopokea mshahara kila tarehe 28 basi wanaposaini mkataba na timu wajue kuwa mwalimu atawachagua muda wowote ule ufaao na usiofaa wawe na uatayari wa kutumikia klabu na sio furaha zao”

“kila mchezaji lazima aniridhishe mazoezin ili nifayne maamuzi sahihi”

“klabu inaniamini na imenipa nafasi hii kubwa. Niamini mimi hakuna atakaye isaliti kwa sababu ya mchezaji kukosa furaha. Ikitokea hivyo basi niatenda nyumbani”

“Nilicheza mpira kwa sababu nilipenda hisia za kucheza soka. Mimi ni mwalimu ili kila mchezaji afurahie kile nilichofurahia mimi”

Tottenham ipo tayari kumtoa Alderweireld nje ya England.

Jermaine Jenas amesema kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Ajax ndoto zake ni kucheza united.

“Spurs kwa asilimia 100 tunamhitaji sana Toby. Davinson Sanchez ni mchezaji mzuri sana lakini hamfikii Toby,” Jenas

“Toby na Jan [Vertonghen] unaweza ukawa muunganiko namba mbili bora zaidi duniani kwa sasa

“Bila shaka Raphael Varane na Sergio Ramos [ Real Madrid], wanaweza wakawa namba moja.

kuhusu yeye kwenda United wametaka £60million lakini wanaweza kujikuta wanampoteza kwa £25million januari.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here