Home Kitaifa Rabbin Sanga akamilisha majaribio, aagwa Uturuki

Rabbin Sanga akamilisha majaribio, aagwa Uturuki

4150
0

Rabbin Sanga amekamilisha majaribio yake hii leo katika Academy ya Besiktas ikiwa ametumia siku 5 badala ya 10 zilizotajwa awali kutokana na uwezo aliouonesha hasa muunganiko na wenzake wa kikosi cha U16 alichokuwa anafanya nacho mazoezi.

Hivyo Sanga anatarajia kurejea Tanzania siku ya Jumapili na Jumatatu atajiunga na timu ya taifa ya vijana kama ilivyoagizwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Ammy Ninje hapo jana.

Sanga ameagwa vizuri na wachezaji wenzake kutokana na mahusiano yao mazuri katika kipindi kifupi.

Shukrani za pekee ziende kwa kampuni ya Beko waliowezesha na kuratibu majaribio haya ya Rabbin Sanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here