Home Kitaifa Rais wa TFF Wallace Karia alivyoguswa na kifo cha Ruge

Rais wa TFF Wallace Karia alivyoguswa na kifo cha Ruge

2441
0

Wadau kibao wamekuwa wanaelezea namna walivyoguswa na kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba. Kwa sababu Ruge alikuwa mwanamichezo, Rais wa TFF Wallace Karia pia ameeleza namna alivyoguswa na msiba huo.

“Ruge nilimfahamu kupitia vyombo vya habari lakini mara ya kwanza kukutana uso kwa uso mimi nilikuwa Mgurugenzi wa Manispaa ya Bukoba na alikuja Bukoba kwenye harakati zake za kuhamasisha vijana kujitambua”-Wallace Karia, Rais TFF.

“Nilikutana nae tukaongea mambo mengi na kuna mambo ambayo tuliongea ambayo yaligusa tasnia yetu ya mpira wa miguu. Ni kijana ambaye alikuwa na vision lakini pia ukizungumza naye anakupa moyo wa kujiamini kufanya kile unachokiamini na sio kulalamika.”

“Baadaye tuliendelea kuwasiliana (siyo kwa karibu sana) kwa shughuli mbalimbali ambazo zilikuwa zinahusiana na burudani, habari na soka.”

“Clouds kama chombo cha habari tunafanyanacho kazi kwa karibu sana na hata wakati fulani niliweza kuleta ugeni mkubwa sana pale Clouds baada ya kuongea na yeye na Shaffih Dauda tukampeleka Rais wa CAF Ahmad Ahmad kwenye tuzo za Ndondo Cup 2018.”

“Lakini yote hayo ni kutokana na ushawishi wake na tuliona mtu ambaye tunaweza kufanyanae kazi pamoja na taasisi yake ambayo tunafanyanayo kazi kwa karibu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here