Home Kitaifa RC Mwanza kuwa wa kwanza kujisajili Rock City Marathon

RC Mwanza kuwa wa kwanza kujisajili Rock City Marathon

6150
0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella anatarajiwa kupamba uzinduzi wa usajili wa mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa unaotarajiwa kuanza Septemba 1 katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu katika Uwanja vya CCM Kirumba  jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya Capitial Plus Internantional,  Bw. Zenno Ngowi, RC Mongella ndiye atakuwa wa kwanza kujisajili katika mbio hizo akiwakilisha wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga na  Simiyu.

“Zoezi hilo la usajili litaanza rasmi Septemba 1 katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo Igoma, Buzuruga, Airport Mwanza, Rock City Mall, Chuo Kikuu cha SAUT, Nyegezi Stand, Mwanza Hotel, Nyamagana Stadium, Dampo pamoja na Nyakato.

Alisema usajili huo pia utahusisha ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.

“Mwaka huu tumeongeza idadi ya vituo vya usajili wa mbio hizi lengo likiwa ni kuwafikia washiriki wengi zaidi ambapo pia kwa upande wa Dar es Salaam usajili utafanyika maeneo ya Mlimani City Vodashop, Vodacom Tower barabara ya Bagamoyo, Masaki Vodashop na Vodashop Arusha,’’ alisema.

Mbio hizo zinazolenga kutangaza Utalii wa Kanda ya Ziwa zimefanikiwa kuvutia wadhamini kadhaa wakiwemo kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper, Vodacom Tanzania, NMB, Tawa, Tanapa, TTB, NSSF, SDS, Gold Crest, New Mwanza Hotel, CF Hospital, CocaCola, Metro FM, EF Outdoor, Tonito , KK Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Link.

Aliongeza kuwa katika kurahisisha zaidi zoezi hilo, usajili wa mwaka huu pia utafanyika kwa njia ya simu kupitia huduma ya M-Pesa.

“Tupo kwenye hatua za mwisho kuhakikisha kwamba washiriki wa mbio hizo wanaweza kujisajili kupitia huduma ya M-PESA ili kuokoa muda na kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi na zaidi linahusisha eneo kubwa la nchi kwa kuwa huduma ya M-PESA inapatikana kila kona ya nchi,’’ alisema.

Alisema usajili huo utahusisha mbio za km 42 kwa wanaume na wanawake, Kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, km 5 kwa washiriki kutoka kwenye mashirika (Corporates) na walemavu wa ngozi, km 3 kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 55 na kuendelea pamoja na km 2.5 kwa watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 10.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here