Home Uncategorized Regnald Mengi ateuliwa na TFF kuwa mlezi wa Serengeti boys

Regnald Mengi ateuliwa na TFF kuwa mlezi wa Serengeti boys

8925
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)leo Jumanne Septemba 4,2018 limemtangaza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ndugu Reginald Mengi kuwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys”

Ndugu Mengi amekuwa akiifuatilia kwa karibu timu hiyo na amekuwa mmoja wa wadau wakubwa wa soka la Vijana.

Amekuwa ni mpenda maendeleo ya mpira wa Miguu hususani soka la Vijana na amekuwa shabiki mkubwa wa Serengeti Boys.

TFF tunaamini tutashirikiana vizuri na Ndugu Mengi katika maendeleo na ustawi wa soka la Vijana.

Ndugu Mengi ni mwanamichezo ambaye hakika amekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza soka la Vijana.

Mara kadhaa amekuwa akiwasiliana na TFF kufuatilia maendeleo ya timu ya Taifa ya U17 kwenye mashindano mbalimbali.

TFF tunafarijika kwa Ndugu Mengi kukubali kuwa mlezi wa timu hii ya Serengeti Boys na tunaamini kwa pamoja tutaifanya timu hii kuwa msingi mzuri katika maendeleo ya ustawi wa soka la Vijana.


Chanzo cha habari TFF

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here