Home Ligi EPL Rekodi walizoweka Wahispania hapo jana Wembley, na habari mpya kuhusu Luke Shaw

Rekodi walizoweka Wahispania hapo jana Wembley, na habari mpya kuhusu Luke Shaw

10881
0

England 1 Hispania 2.

Marcus Rashford alitangulia kuifungia Uingereza bao la kwanza dakika ya 11 bao ambalo lilidumu kwa dakika mbili tu baada ya Saul Niguez kusawazisha dakika ya 13 na kisha Rodrigo kuifungia Hispania la pili dakika ya 31.

Kwanza kabisa kabla hata ya mchezo ule kuanza Wahispania walienda Wembley wakiwa na matumaini, kwani katika michezo 6 kabla ya ule wa jana Wahispania walipoteza mechi 1 tu.

Hii ina maana baada ya michezo 7 sasa na ule wa jana, Hispania anakuwa amemfunga Muingereza mara 5 huku Waingereza wakiambulia suluhu 1 tu na huo ushindi wao mmoja.

Mlinzi wa kushoto wa Hispania Marcos Alonso jana alifanikiwa kuanza katika kikosi cha timu ya taifa Hispaniana hii ikiwa ni baada ya miaka 37 na siku 167 baada ya baba yake kuichezea Hispania(na ilikuwa vs Uingereza Wembley).

Timu ya taifa Hispania imeanza kuona mwanga mpya kwenye ushambuliaji, ni Rodrigo Moreno ambapo kwa bao alilowafunga Waingereza sasa anakuwa amehusika katika mabao 4 katika timu ya taifa(assists 1 na mabao 3).

Kwa matokeo yale ya jana sasa Hispania wanakuwa wameshind michezo miwili Wembley na huku michezo yote hiyo ikiihusisha familia ya wakina Alonso( 1981 alikuwa baba Alonso na jana alikuwa Alonso mwenyewe).

Lakini pia kocha wa Uingereza Gareth Southgate huu ndio ulikuwa mchezo wake wa kwanza kupoteza katika dimba la Wembley, katika uwanja huu ameshinda mara 6 na kutoka suluhu mara 4.

Lakini kuhusu tukio lililotokea katika mchezo huo la Luke Shaw kuumia vibaya, hii leo ameweza kutweet na kuwaambia mashabiki zake kwamba “musihofu yuko salama na atapambana arudi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here