Home Ligi EPL Rekodi zinaibeba Chelsea kuipiga Man City ngao ya hisani

Rekodi zinaibeba Chelsea kuipiga Man City ngao ya hisani

14132
0

Kwa mara ya kwanza Maurizio Sarri na Jorginho watakuwa uwanjani Wembley kuiwakilisha Chelsea katika mchezo wa ngao ya hisani wakati Chelsea watakapokipiga dhidi ya Man City.

Kulikuwa na hofu kwamba huenda mchezaji mpya wa City Ryad Mahrez asiwepo katika mchezo huo kutokana na majeruhi lakini Pep Gurdiola amesema Mahrez anaweza kuanza dhidi ya Chelsea.

Man City wataingia katika mchezo huu bila ya huduma ya nyota wao kadhaa akiwemo Kelvin De Bruyne na Raheem Sterling walioko likizo huku Chelsea wakiwakosa Hazard, Courtois, Batshuayi, Kante na Giroud ambao nao bado hawajarudi.

Mara ya mwisho kwa klabu ya Manchester City kubeba ngao ya hisani ilikuwa mwaka 2012 ambapo City waliipiga Chelsea goli 3-2 japo mwaka huo mchezo huu ulipigwa Villa Park badala ya Wembeley.

Kwa Chelsea wenyewe mara yao ya mwisho kubeba ngao ya hisani ilikuwa mwaka 2009 ambapo walifanikiwa kuifunga Manchester United kwa mikwaju 4-1 ya penati katika dimba la Wembley.

Tayari Chelsea wameshapoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya City iliyopita, lakini tangu September mwaka 2010 Chelsea hawajawahi kupoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya Man City.

Takwimu zinaonesha kwamba katika mechi nne zilizopita za ngao ya hisani, bingwa wa kombe la FA ndio alifanikiwa kubeba ngao hii huku Manchester United wakiwa mabingwa wa mwisho wa ligi kubeba ngao hiyo.

Mwaka 1970 ilikuwa mara ya mwisho kwa Man City kushinda mechi tatu mfululizo Wembley, mechi zao mbili zilizopita Wembley wameshinda zote moja wakiipiga Spurs 3-1, kisha Arsenal 3-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here