Home Ligi EPL Robinho afunguka Real Madrid walivyoikomoa Chelsea kupitia Man City

Robinho afunguka Real Madrid walivyoikomoa Chelsea kupitia Man City

10973
0

Mwaka 2008 klabu ya soka ya Real Madrid waliamua kumuuza mshambuliaji wao wa Kibrazil Robinho kwenda katika klabu ya Manchester City kwa ada ya £32m.

Usajili wa Robinho kwenda Man City haukufikiriwa na wengi kwani iliaminika anaweza akaenda Chelsea kutokana na tetesi zilivyokuwa nyingi zikimhusisha kutia darajani.

Miaka takribani 10 imepita na hatimaye Robinho mwenyewe ameeleza nini kilichotokea wakati wa usajili wake kwenda City na akisema yeye mwenyewe alitamani kwenda Chelsea.

Robinho anasema wakati ule hakuwa anawaza sana kuhusu Man City kwani hawakuwepo Champions League tofauti na Chelsea.

Nini kilikwamisha yeye kujiunga na Chelsea?

“Mabosi wa Real Madrid walikasirishwa sana na kitendo cha Chelsea kuanza kutengeneza jezi zenye jina langu na mashabiki zao kuanza kuzivaa”

Baada ya Real kuona Chelsea wamefanya jambo hilo ndipo wakaamua kuua biashara kati yao kuhusu Robinho na wakaamua kumuuza Manchester City.

Robinho amesema pia hajutii kuondoka Madrid lakini anasikitika walivyokuwa na mwisho mbaya, na namna alivyoondoka inaweza kuwafanya wakasahau mema yote aliyowatendea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here