Home Kimataifa Ronaldo aitosa Ureno ili kujifua zaidi na Juventus

Ronaldo aitosa Ureno ili kujifua zaidi na Juventus

14302
0

Cristiano Ronaldo amepatwa na tatizo kwenye jicho lake la kushoto na kuamua kuachana na timu yake ya taifa kwa muda.
Mchezaji huyo wa Portugal baada ya kuanza vibaya na Juventus ameamua kupumzika na timu ya taifa ili kutumia muda mwingi wa mazoezi na klabu yake ya  Juventus. Cristiano Ronaldo amedai kuwa anajiandaa kisawasawa na Juventus hivyo ameona asiende Ureno kwa sasa.

Wachezaji wenzake wanajiandaa na mtanange wao dhidi ya Croatia na Italy, lakini Ronaldo amebaki mjini Turin pamoja na Sami Khedira, aliyetemwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa. Ronaldo alipatwa na maumivu kwenye mchezo wake dhidi ya Parma
Kocha mkuu wa Ureno Fernando Santos alielezea kuwa kutokujumuishwa kwa  Ronaldo ni kwa muda tu.

‘Nimeongea na Ronaldo, ameniambia tokea amejiunga na Juventus bado hajazoea mazingira. Bado anahitaji muda mwingi na kufanya mazoezi ya kutosha na klabuni”

Ureno wanajiandaa na  UEFA Nations League.

Ronaldo anatarajia kurudi timu ya taifa mwezi wa 10 kwenye mchezo wao dhidi ya Scotland.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here