Home Uncategorized Rooney amtaja anayepaswa kubeba lawama kiwango cha Pogba, sio Mourinho

Rooney amtaja anayepaswa kubeba lawama kiwango cha Pogba, sio Mourinho

11458
0

Kumekuwa na maneno mengi kuhusu kiwango cha kiungo wa Manchester United Paul Pogba, huku wengi wakimshambulia kutokana na kiwango anachoonesha akiwa na Manchester United.

Kila mtu amekuwa na maoni yake kuhusu kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa lakini wengi wamekuwa wakimshtumu Jose Mourinho kuwa sababu ya kushuka kwa kiwango cha Pogba.

Wengi wanasema Mourinho kwa namna anavyomtumia Paul Pogba akiwa United inamuwia ngumu kiungo huyo kuonesha kiwango anachoonesha akiwa Ufaransa au alipokuwa Juventus.

Lakini mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney ameibuka na kusema kwamba Jose Mourinho hapaswi kulaumiwa kwa kiwango kibovu cha Pogba.

Rooney ambaye alifunga jumla ya mabao 253 katika miaka 13 aliyoichezea United amesema Pogba mwenyewe ndiye anapaswa kulaumiwa kuhusu kiwango anachoonesha United.

Wayne amesisitiza kwamba Pogba ni kiungo mwenye kiwango cha dunia na kwa level yake yeye ndio anapaswa kutafuta namna ya kurejesha makali yake akiwa United na sio mtu mwingine kumfanyia hivyo.

“Unakaa unawasikia watu wakisema Mourinho anapaswa kumuweka Paul katika kiwango chake, lakini sio hivyo. Ni Pogba mwenyewe anapaswa kupambania suala hilo” alisema Rooney.

Katika hatua nyingine kocha wa Manchester United amegoma kujadili hali ya Paul Pogba klabuni hapo, huku nje tetesi zikizidi kukua kwamba Pogba na United kuna mpasuko. United watakuwa uwanjani kesho kuwakabili Tottenham katoka muendelezo wa EPL.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here