Home Kimataifa Rooney azidi kung’ara, Ac Milan yamnasa nyota wa Uruguay

Rooney azidi kung’ara, Ac Milan yamnasa nyota wa Uruguay

8802
0

Crystal Palace wamepoteza michezo miwili kati ya 22 ya Premier League ambayo Wilfried Zaha amefunga bao:

• 15 ushindi
• 5 sare
• 2 walizopoteza
23 Mabao aliyoifungia klabu hiyo

Tarehe kama ya leo 2003, Cristiano Ronaldo aliichezea Manchester United Mechi yake ya kwanza kabisa vs. Bolton.

• 292 Michezo
• 118 Mabao
• 9 Makombe

Wayne Rooney amehusika katika mabao 6 kwenye michezo yake 7 kwa DC United katika ligi kuu ya MLS Msimu huu

3 Mabao ⚽
3 Asisti 🅰️

Kiungo wa klabu ya Juventus, Miralem Pjanic, anatarajia kuongeza kuongeza mkataba mpya na klabu ya Juventus. Pjanic, atasaini mkataba mpya ambao utakaomfanya abaki katika klabu hiyo mpaka mwaka 2022 na atakuwa akilipiwa mshahara kwa mwaka paundi million 7.
Pjanic, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuondoka Karola klabu hiyo na kujiunga na baadhi za timu kama Real Madrid, Paris Saint Germain, Barcelona, na Manchester City, lakini Juventus, walitaka kiasi cha paundi million 100 ili kumuachia kiungo huyo.

Beki wa klabu ya Genoa, Diego Laxalt, amewasili jijini Milan, kufanyiwa vipimo vya afya na kujiunga na klabu ya Ac Milan.
Ac Milan, wamefikia makubaliano ya kulipa ada ya uhamisho wa paundi million 14 na wapo tayari kuongeza bonus ya paundi million 4 kama beki huyo akicheza kiwango cha juu. Laxalt, msimu uliopita amechezea Genoa, michezo 34 na kufunga mabao 4.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here