Home Kitaifa Rostand safari imeiva Yanga

Rostand safari imeiva Yanga

10040
0

Hatma ya Youthe Rostand itajulikana wakati wowote kuanzia sasa ndani ya Yanga. Inaelezwa uongozi wa timu hiyo upo katika mipango ya kumpiga chini kuelekea msimu ujao wa 2018/19.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga Hussein Nyika amesema kamati ya usajili inajadili mustakabali wake huku Youthe akiwa hajasafiri na timu kwenda Morogoro kwenye kambi ya maandalizi.

“Kamati ya usajili tuna kikao kwa ajili ya kuangalia mustakabali wa golikipa huyo na bahati nzuri hakuwa sehemu ya kikosi kilichoenda Morogoro. Siwezi kulitolea taarifa sasa hivi mpaka tutakapokutana na kamati nzima tutatoa maamuzi wanahabari watafahamishwa pamoja na umma wa wanayanga.”

“Tutakapokua tumefanya maamuzi tutatangaza kama ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga au ataenda sehemu kwa mkopo kwa sababu sehemu nyingine madirisha bado yapo wazi ndio maana hakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji waliokwenda Morogoro.”

“Tumeshaanza maongezi na mchezaji mwenyewe tumemsikiliza mawazo na ushauri wake  tutakaa kama jopo na sisi kutoa maamuzi kama viongozi itakapofikia mwafaka watu watajua.”

“Ukiwa kama mwanahabari za michezo umeshaona tumefanya usajili wa golikipa mwingine toka Congo DR, hiyo tu inalnesha kuna kitu kwa sababu huwezi kuwa na magolikipa wawili wakigeni mbaya zaidi huwezi kuwa na magolikipa wanne kwenye timu.”

“Hivyo vitu vyote lazima mwelekeo, kama viongozi wa Yanga na technical bench ni nini walichoamua kukifanya atolewe kwa mkopo au  kuvunja mkataba, hivyo ni vitu vinavyojulikana.”

“Kiwango chake sio kama tulivyomchukua mwanzo, kimezidj kushuka kila siku kwa hiyo ndio maana benchi la ufundi likashauri atafutwe golikipa mwingine.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here