Home Kitaifa Rotary Dar Marathon yaadhimisha miaka kumi ya kubadilisha maisha

Rotary Dar Marathon yaadhimisha miaka kumi ya kubadilisha maisha

7488
0
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon wakifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wikiendi hii jijini Dar es Salaam ambapo walitangaza rasmi maandalizi ya matembezi hayo kwa mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika tarehe Oktoba 14, mwaka huu. Mbio za Rotary Dar zitaanza na kuishia katika viwanja vya ‘The Green’, Oysterbay.

Tukio maarufu la riadha la Rotary Dar Marathon ambalo hufanyika siku ya 14 Oktoba – siku ya Nyerere kila mwaka tangu 2009 litaadhimisha mwaka wa kumi tangu kuanza kwa tukio hilo. Dhima ya Rotary Dar Marathon inaendelea kuwa “ponya maisha, badilisha jamii” na ni katika mwaka wa tatu tangu RDM imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za hospitali ya (CCBRT) kuwa na mradi wa hsopitali binafsi ili waweze kupunguza gharama ya hudua za ulemavu zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wana jamii.  Fedha zote zitakazokusanywa mwaka huu kutokana na tukio la RDM zitakabidhiwa kwa CCBRT ili kukamilisha ujenzi wa kliniki hiyo binafsi na manunuzi ya vifaa husika.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Rotarian Catherinerose Barreto, alisema kwamba kamati inayojumuisha wajumbe kutoka klabu nane za Rotary za jijini Dar es Salaam imeshaanza maandalizi kuhakikisha mwaka huu RDM inakuwa tukio ambalo ni la ubora wa hali ya juu. Aliongeza pia mlezi wa RDM Mheshimiwa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi atakuwepo na kushiriki matembezi ya siku hiyo.

Mkuu wa kitengo cha ruti za Rotary Dar Marathon, Diamond Carvalho akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Mbio hizo zitajumuisha matembezi ya kifamilia ya kujifurahisha ya kilomita 5 na 9, mashindano ya riadha na baiskeli ya kilomita 21.1 na 42.2.

Tukio la Rotary Dar Marathon (RDM) licha ya kulenga lengo msingi la kuchangisha fedha kusaidia shughuli mbalimbali ili kuboresha ubora wa maisha kwa jamii zetu pia linahakikisha kutoa tukio lenye ubora wa kimataifa na la kufurahiwa na wanaoshiriki katika mbio au matembezi. Kila mwaka RDM inachukua hatua za ziada kuhakikisha tukio linafanyika katika kiwango cha juu ili washiriki wote ambao ni wanariadha wataalamu na wengineo wanafurahia siku hiyo na pia kuweza kutumia shindano kama njia ya kuongeza uzoefu wao na kukua katika michezo wa riadha.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Hawa Mkwela akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.

Mkuu wa njia za RDM Rotarian Diamond Carvallo, naye alisema kwamba anatarajia tukio la mwaka kuvutia washiriki ya zaidi 16,000, na baadhi pia inatarajiwa kuwa baadhi ya washiriki watakuja kutoka nje ya nchi. Katika tukio la RDM mwaka huu kutakuwa na mashinda ya riadha na baiskeli kwa kilomita 21.1km na 42.2  vilevile matembezi ya kujifurahisha ya kilomita  5 na 9. Riadha na matembezi yote yataanzia na kumalizika katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Gavana wa Rotary na mwenyekiti wa RDM, Sharmila Bhatt aliongeza, “ni sera yetu kufanya kazi kwa pamoja na mashirika mbalimbali katika juhudi zetu za kuleta mabadiliko katika katika jamii zetu. Tunaamini kwamba kufanya kazi pamoja kutaleta mafanikio makubwa katika jamii kwa ujumla. Tunapenda kuwashukuru Bank M kwa kushirikiana nasi kwa miaka tisa iliyopita na SBC – Pepsi kwa kuendelea na udhamini wao Tshirts,-vinywaji na mwaka huu kwa kuongeza msaada zaidi katika kufanikisha RDM. Mwaka huu tutakuwa washirika wapya na tunafurahi sana kuweza kuleta tukio la Rotary Dar Marathon mwaka huu hii ikiwa ni tukio letu la 10.”

Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon, Sharmila Bhatt akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Rotary Dar Marathon inatarajia kuwavutia washiriki 16,000 kwa mwaka huu.

Kwa miaka 9 iliyopita, Rotary Dar Marathon imeendeleza miradi kadhaa kama vile kupanda miti 27,000, kutoa vifaa vya maji na usafi wa mazingira kwa shule 27, kujenga wodi ya watoto ya saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia kukarabati na kuweka vifaa katika kituo cha ujasiriamali cha Rotary katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here