Home Kimataifa Sakata la mwamuzi kupewa rushwa Rwanda katika sura nyingine

Sakata la mwamuzi kupewa rushwa Rwanda katika sura nyingine

13616
0

Viongozi wa FERWAFA (Katibu Mkuu wa FERWAFA Francois Regis Uwayezu na kamishna wa mashindano Eric Ruhamiza) wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa waamuzi waliochezesha mechi kati ya Rwanda dhidi ya Ivory Coast ili kupanga matokeo inasemekana fedha walizozitoa haikuwa ni rushwa bali walikuwa wanalipa gharama za safari za waamuzi hao.

Inaelezwa baada ya waamuzi hao kufika Rwanda toka Namibia kuna gharama ambazo zilizidi na ilitakiwa kulipwa na chama cha soka cha Rwanda FERWAFA na waamuzi hao waliomba kurejeshewa gharama hizo.

Lakini viongozi hao wa wanashangaa kwa sababu gani wanatuhumiwa kwa rushwa na kutaka kupanga matokeo ikiwa waamuzi wa mchezo huo waliomba kurudishiwa gharama zao (fidia) jambo ambalo ni kawaida.

Mwamuzi wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mkufunzi wa waamuzi anaetambuliwa na Caf Leslie Liunda ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa waamuzi kulipwa fidia ya gharama za safari.

“Utaratibu uliopo sasa hivi Caf wanateua waamuzi kwenda kuchezesha mashindano mbalimbali ambayo wanayatambua, wanapokuwa wanateuliwa yale mafao au malipo yanayotokana na kazi wanayokwenda kuifanya yanafanywa na Caf baada ya waamuzi kwenda kuchezesha.”

“Wakati huohuo Caf wenyewe au vyama husika kulingana na aina ya mashindano wanalazimika kuwatumia tiketi waamuzi kutoka nchi moja kwenda nchi wanayokwenda kuchezesha. Safari hizo zinatakiwa zianzie kwenye miji mikuu au ndege zinapoanzia katika miji husika kama Tanzania kwa mfano waamuzi wanakwenda kuchezesha Burundi safari yao itaanzia Dar es Salaam.”

“Waamuzi watakaokuwa wanatoka nje ya Dar es Salaam wanatakiwa wajigharamie wenyewe kutoka wanapotoka hadi Dar na kuelekea kwenye mchezo wao. Pindi watakapofika kwenye mchezo wao, chama cha mpira cha nchi husikaki kitatakiwa kiwarudishie gharama ambazo watakuwa wamezifanya wakiwa safarini kuelekea kwenye mchezo huo.”

“Kama kuna malalamiko ya tuhuma za namna hiyo, Caf watafanya utaratibu wa kufanya uchunguzi kwa sababu ipo idara inayoshughulika na mambo kama hayo kufatilia na kujua.”

“Kwa hali ya kawaida kama leo tumekwenda katika mchezo, waamuzi wakafatwa na mtu au watu au chama cha mpira mhusika mkuu wa Caf kwa wakati huo anakuwa kamishna wa mchezo kwa hiyo wanatakiwa suala hilo waliripoti kwa kamishna wa mchezo, assessor au coordinator wanatakiwa wafahamu na hao ndio watoe taarifa kwa Caf.”

“Kama wametoa taarifa kwa kamishna lakini hawajapata ushirikiano basi wanaripoti wenyewe moja kwa moja Caf na wataambiwa nini cha kufanya kuhusiana na tuhuma husika.”

Watuhumiwa wote wanashikiliwa katika kituo cha poilisi cha Kimihurura kwa mujibu wa Rwanda Investigations Bureau.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here