Home Kimataifa Salamba angalizie kwa Kaheza ukishindwa kwa Ambokile.

Salamba angalizie kwa Kaheza ukishindwa kwa Ambokile.

4540
0

Makala na Raphael LucasMiaka kadhaa iliyopita maeneo ya Kakola wilayani Kahama aliibuka kijana mwenye nguvu na uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu za wapinzani pasipo kujali ni mazingira yapi ya uwanja na ulinzi wa mabeki upo juu ake nae ni Adam Salamba. Kijana mwenye juhudi binafsi asiye na nafasi ya kujinasua mbele ya utakatifu wa Bocco,Okwi na Kagere pale Simba.Salamba amekulia kimpira ndani ya kikosi cha wachimba dhahabu wa Bulyanhulu wanaoshiriki ligi daraja la pili Tanzania Bara, nakumbuka juhudi zake binafsi kwani binafsi nimefanikiwa kuona makuzi yake ya kisoka kwenye uwanja wa shule ya msingi Kakola b akiwa na bulyanhulu na baada ya hapo alipata nafasi ya kuchezea timu ya Taifa ya maboresho safari ilofungua milango ya kutoka wilayani na kufika mkoani yaani ndani ya kikosi cha wapiga debe wa Shinyanga Stand United.Salamba hakuhudumu sana kwenye kikosi cha wapiga debe hao na hatimaye alitimukia Lipuli Fc ya Iringa ambako kwa mda mfupi alionesha uwezo wake wa kufunga mabao kwenye viwanja vyote kuanzia kwa mchina hadi viwanja vya mikoani na kufanikisha kufunga mabao zaidi ya kumi kwa msimu uliopita.Baada ya kuonesha uwezo huo Yanga waliomba huduma ya Salamba kutoka Lipuli iwasaidie kujinasua kutoka kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika na ombi lao kugonga Mwamba, Baada ya hapo Salamba akaona na kuhisi Yanga sio sehemu sahihi kwa maendeleo ya soka lake la kupachika mabao na kuelekea ndani ya kikosi cha Simba na usajiri wake ukiibua gumzo kubwa mitandaoni.Salamba akajikuta kwenye wakati mgumu zaidi hasa juu ya ubora wa Bocco, Okwi na Kagere na kumfanya aendelee kusubiri benchi mpaka pale watatu hao watahitajika kupumzishwa nae apate nafasi, wakati huo huo Marcel Kaheza alikua anasumbukia kupata nafasi pale msimbazi na kuamua kutimkia Kenya kwa mkopo huku Salamba akiamini ipo siku atatoboa pale SimbaKutokana na Sera na mikakati ya Simba sioni nafasi ya Salamba, Mlipili, Kaheza kupata nafasi kubwa ya kupata uzoefu wa mashindano kwani bado ni vijana wadogo kisoka ambao wanatakiwa kupewa mda mwingi wa kujifunza ikiwa Simba haina mda huo ni wakati muafaka wa Salamba kujifunza kutoka kwa Kaheza aliyepo kwa mkopo nchini kenya au atafte club itayompa mda mwingi kujenga kiwango chake kama ilivyokua kwa Ambokile aliyetimukia kwa mkopo nchini Afrika kusini kwenye kikosi cha Fc Leopards pasipo kua na mawazo ya Simba na Yanga na ndio maana Leo yupo huko. Sipo kuwaaminisha Salamba ni bora kuliko Bocco lakini anaweza tengenezwa kua Bocco mwingine au Samata wa Simba Tanzania.“Salamba kumbuka Kakola wanahitaji kukuona Taifa stars na sio kwenye benchi la akiba la Simba”Raphael Lucas (udom)0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here