Home Uncategorized Salum Kihimbwa amwaga wino Mtibwa

Salum Kihimbwa amwaga wino Mtibwa

9534
0

Salum Kihimbwa baada ya kuitwa timu ya taifa ameongeza mkataba na klabu yake ya Mtibwa. Salum Kihimbwa aliyezaliwa desemba 20 mwaka 1997 ni Mchezaji mwenye kipaji kipekee amemwaga wino wa kuendelea kuitumikia klabu yake.

Baada ya kuongeza kandarasi hiyo Kihimbwa amesema ana furaha klabuni hapo na ana amini kuwa klabu yake bado ina uwezo wa kutetea taji la FA na bado ana uhakika wa kufanya vizuri msimu huu. Hana wasiwasi kabisa na uwezo wa timu yake. Anachokiamini kuwa Mtibwa ina uwezo wa kupambana katika michezo yote 19.


Timu yetu ina wachezaji wengi sana na wenye uwzo mkubwa. Hii inasadifu kwamba lazima tupambane ili uweze kupata nafasi” Kihimbwa


Pia Kihimbwa alizungumzia mipango ya klabu yake msimu huu

“Sisi wachezaji tunapambana kuhakikisha kuwa tunatimiza malengo ya klabu. Nina imani kuwa kila mchezaji wa Mtibwa hatutawaangusha mashabiki wetu”

Kihimbwa amesaini mkataba wa miaka miwili. Huu ulikuwa msimu wake wa pili ndani ya klabu hiyo ambayo ilimsajili na kumtambulisha ligi kuu.

Julai 31 Salum Ramadhani Kihimbwa aliafikiana na klabu ya Mtibwa kuwa ataongeza mkataba wa miaka 2 Mtibwa Sugar. Mkataba wake awali ulibakia mwaka mmoja na sasa amesaini miaka 2 mbele na kuufanya mkataba wake kuwa wa miaka 3, hivyo mkataba utafika tamati katika msimu wa 2020/2021


Hivi majuzi Stars inayofundishwa na nyota wa zamani wa Nigeria Emanuel Amunike aliwaita katika kikosi chake mshambuliaji Kelvin Sabato Kongwe na kiungo mshambuliaji Salum Ramadhani Kihimbwa.

Kupitia mmoja wa watendaji wa klabu ya Mtibwa Sugar Swabr Abubakar alisema ni jambo la kheri Mtibwa Sugar kutoa mchango kwa taifa.

Katika kikosi cha awali kilichotajwa Agosti 21 wachezaji hawa hawakuwemo katika wachezaji 25 waliotajwa lakini kocha mkuu wa timu ya taifa amewafuatilia wachezaji hawa katika michezo yao na kuamua kuwaita katika kikosi cha Stars.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here