Home Kimataifa Samatta azidi kupaa ufungaji bora Ubelgiji

Samatta azidi kupaa ufungaji bora Ubelgiji

4806
0

Mbwana Samatta anaendelea kukifukuzia kiatu cha ufungaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Jupiler Pro League) baada ya usiku wa Ijumaa February 8, 2019 kupachika mabao mawili kambani wakati KRC Genk ikishinda nyumbani 2-0 dhidi ya Standard Liege.

Magoli hayo mawili yanamfanya Samatta kufikisha jumla ya magoli 19 kwenye ligi msimu huu na kuendelea kumuacha mpinzani wake Hamdi Harbaoui mwenye magoli 14.

Samatta amefunga magoli hayo dhidi ya golikipa maarufu wa Mexico Guillermo Ochoa ambaye alikuwepo kwenye fainali nne (2006, 2010, 2014 na 2018) za michuano ya kombe la dunia.

Ushindi wa Genk unaifanya timu hiyo iendelee kujitanua kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza michezo 25 ikizipiga bao Club Brugge na Royal Antwerp zenye pointi 45 katika nafasi ya pili na ya tatu zikiwa zimecheza michezo 24 kila moja.

Ligi hiyo yenye timu 16, hadi sasa Genk imebakiza michezo mitano kabla ligi haijamalizika kwa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here