Home Kimataifa Sanchez alibet £20,000 Mourinho kufukuzwa

Sanchez alibet £20,000 Mourinho kufukuzwa

4649
0

Kumbe walio wengi United hawakumtaka Mourinho. Taarifa za kidukuzi zinasema kuwa baadhi ya wachezaji walikuwa wakishindana kwenye kundi lao la Whatsapp juu ya hatma ya Mourinho.

Inasemekana kuwa Sanchez ambaye ndiye mchezaji anyeongoza kikosini hapo kwa mshahara mnono zaidi (£450,000) aliwaambia wachezaji wenzake wawe wavumilivu mambo yatakaa sawa. Mara baada ya Mourinho kutimuliwa Sanchez alimwambia Marcos Rojo kuwa naomba £20,000 yangu. Kiasi hicho cha pesa ni sawa na Tsh Milioni 58.

Ujumbe huo uliashiria kuwa Rojo na Sanchez walibet juu ya hatma ya Mou ndipo Sanchez akaibuka mshindi na kumtaka Rojo amlipe kiasi ambacho walikubaliana.

Kwa taarifa hiyo sidhani kama Mourinho alibakiza rafiki tena ugani Old Trafford zaidi ya Lukaku ambaye inasemekana hajaungana sana na wenzake katika kufurahia kuondoshwa kwa Mou.

Sanchez alisakamwa na kiwango kibovu sana OT ambapo katika michezo 30 alifunga magoli 4 tu chini ya Mou.

Hata hivyo inasadikika kuwa Sanchez na mshambuliaji mwenzake Romelu Lukaku wataukosa mchezo ujao dhidi ya Cardiff kutokana na majeraha.

Kocha huyo mpya pia amesema kuwa Pogba atakuwa ndiye nguzo muhimu kwenye kikosi chake kutokana na uwezo mkubwa alio nao wa kuiunganisha timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here