Home Kimataifa Sanga wa Ndondo Academy ameanza majaribio Uturuki

Sanga wa Ndondo Academy ameanza majaribio Uturuki

4308
0

Leo Rabbin Sanga ameanza majaribio yake kwenye klabu ya Besiktas ya Uturuki ikiwa ni siku ya kwanza kati ya siku 10 ambazo atafanya majaribio.

Sanga amepokelewa vizuri na kufanya mazoezi na timu ya cijana wenye umri wa miaka 16 baadaye wakawapisha vijana wenye miaka chini ya 15 na wakamaliza vijana wa chini ya miaka 14.

Ameanza vizuri pamoja na kwamba hakukuwa na mchezaji yeyote mwingine mwenye asili ya Afrika lakini Sanga aliweza kushirikiananao vizuri wakamfahamu jina na wakawa wanaita wakati wa kupeana pasi.

Baada ya kumaliza mazoezi ya siku ya kwanza, mmoja wa wenyeji wetu katika kituo hicho amesema hakuanza vibaya, ameanza vizuri tofauti na vijana wengine ambao wanafika katika kituo hicho.

Hali ya hewa ya baridi ilikua changamoto kidogo lakini ustadi wake wa kupiga pasi na kumiliki mpira umethibitisha hakuchaguliwa kwa bahati mbaya kuwa mchezaji bora wa #NdondoCupacAdemy

Kesho anaingia siku ya pili ya majaribio.
#NdondoCupAcademy @beko @ndondo_cup @drfa_Tanzania @shadakasports

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here