Home DOKUMENTARI Sarakasi wanazokumbanazo Mabibo FF kuifikia La Masia

Sarakasi wanazokumbanazo Mabibo FF kuifikia La Masia

11633
0

Omary Malungu ni moja ya zao la Mabibo FF. Kwa sasa Omar anayejulikana kama Van Magoli kwa sasa yupo Mtibwa Sugar akiitumikia timu ya vijana. Malungu ni mzaliwa wa Tanga alizaliwa mwaka 2000. Ni kijana mwenye kipaji cha kipekee.

Mabibo FF ilianzishwaje?

Mabibo FF lianzishwa mwezi wa 27 April 2018. Lengo la taasisi hii ni kulea vijana mbalimbali wa mtaani wasio na uwezo wa kuongoza maisha yao ya kisoka ili kufikia malengo na ndoto zao.


Uongozi?

Nilibahatika kuongea na mmoja wa viongozi wa akademi hiyo akanipa muongozo na namna uongozi unavyofanya kazi.

  • Clemence Philip
  • Walter Sembuli
  • Ramadhan Fauka
  • Hamed Makambi
  • Salim Mahimbo
  • Moses Kihenga

Hao wote kwa pamoja ni viongozi na wamiliki wa akademi hiyo.

Historia ya klabu hiyo?

Clemence Philipo akiwa na wenzake kijiweni walianza ubishani kuhusiana na ni mguu upi una umuhimu zaidi uwanjani (kati ya wale wanaotumia mguu wa kushoto na wale wa mguu wa kulia).

“Mimi na Walter tulikubaliana kutengeneza timu mbili moja iwe na wacheza na mguu wa kushoto pekee na timu ya pili wale wanaotumia mguu wa kulia” Alisema Clemence.

“Baadae akajitokeza Ramadhan Fauka ambaye mimi nilikuwa sifahamiani nae lakini nae pia alikuwa na wazo wa kuanzisha timu”

Baada ya wadau hao kukutana basi wakahama kutoka wazo la kuwa na timu ya mguu wa kushoto na kulia wakaamua kutengeneza akademi ya vijana wadogo.

Ahmed Makambi nae akaongezeka ingawa yeye ni mshabiki wa mpira tu sio mchezaji kama Clemence.

Penye nia pana nguvu Mabibo Football Foundation ikaanzishwa. Wakaanza mchakato wao wa kutafuta watoto wanoacheza soka la mtaani wa mitaa yote ya Mabibo. Mwanzoni klabu ilianza na wachezaji 8 pekee.

Utaratibu wa kumuingiza kijana kwenye taasisi upoje?

“Huwa mara nyingi wachezaji wetu wa hapa ndani wanakuwa na mazoea ya kuja na marafiki zao. Lakini huwa hatuwaingizi kwenye akademi moja kwa moja. Kila mtoto akija tunampa nafasi ya kufanya majaribio kwa wiki baada ya hapo utaratibu wa kimkataba unafuata kama anatufaa” Clemence

Malezi na kambi kwa Ujumla?

Kwa mfano akademi za wenzetu kama La Masia watoto huwa wanabaki kambini, wanakula na kulala kambini. Kama unavyokumbuka Lionel Messi aliposajiliwa La Masia 2000 mkataba wake ulisainiwa kwenye tishu ili aweze kujiunga La Masia.

Kwa upande wa Mabibo FF mabosi wa akademi wanawahudumia vijana wao pindi wanapokwama au wanapohitaji matumizi kadhaa ya kisoka kuendana na stahiki zao. Kwakuwa bado kambi yao ni changa hawana kambi maalumu.

“Kwa sasa hatuna hosteli wala kambi maana ndo kwanza tunaanza” Clemence

Mafanikio yao?

Tuliposikia kuna majaribio ya vijana wa umri wa chini ya miaka 20 tulisema ngoja nasi tukajaribu bahati yetu huenda kijana wetu mmoja akafanikiwa. Kweli Mtibwa walikuja Dar es Salaam tukapeleka vijana wetu. walikuwepo vijana zaidi ya 200 waliokuwa wakijaribiwa. Mungu mkubwa vijana wetu wawili wakabaki kati ya hao 200 akiwemo Van Magoli.

Uwanja na mazoezi kwa ujumla?

Wakati wanaanzisha taasisi walikumbwa na changamoto kidogo walikuwa wanafanya mazoezi kwenye uwanja wa chuo cha usafirishaji NIT.

Walipata nafasi ya kuchezea uwanja huo baada ya Afisa michezo mkoa wa Dar es Salaam Adolf Alli kuwaombea kibali kutoka uongozi wa chuo hicho.

Changamoto ya uwanja?

Kufikia mwezi wa 8 wakakumbwa na sintofahamu kutoka kwa uongozinwa chuo hicho wakidai kuwa hawakuwa na kibali maalum. Sababu kubwa ni kwamba timu nyingi zilikuwa zinaomba kuutumia uwanja huo hivyo uongozi wa chuo ukataka kuanzisha utaratibu maalum wa haki za kutumia uwanja huo.

Sababu hasa ni nini?

“Uwanja huo hauna uzio na upo kwenye matengenezo. Baadhi ya vilabu vingine vya mtaani vilikuwa vinaingia ndani yabuwnajan huo na kufanya mazoezi bila kibali. Sasa wakati wa zuio hilo nasi tulijumuishwa kwa sababu hata sisi hatukuwa na vibali maalumu”

Njia mbadala?

“Baadae tukaamua kuandika barua ya maombi. Barua yetu ilipitia serikali za Mitaa,. Lakini katika sakata hilo wakatuambia mpaka tuwajibu, sasa sisi hatukuweza kukaa kimyaa bila kujua cha kufanya kwa sababu tu hatujajibiwa”

“Tukaamua kusogea uwanja mdogo hapa wa makuburi upo maeneo ya kanisani. Tukawa tunaruhusiwa kuutumia kwa muda kwa sababu uwanja huo huo ulikuwa unatumiwa na klabu ya Makuburi FC”

Mkono mtupu haulambwi?

“Ikabidi tutafute wadau na watu wazito wazito ili watusaidie kurudi tena NIT. Timu ya Veteran FC ilianzisha bonanza fulani ambalo hata sie tulishirikishwa. Kwa bahati nzuri katika bonanza lile tukakutana na Meya Jacob Boniface wa Ubongo.

Tukamweleza tatizo letu. Tunamshukuru Meya ni msikivu sana anapenda michezo akatuambia atafuatilia suala letu.

Pia tukafanikiwa pia kukutana na Mzee Kiongoa ambaye ni mmoja wa wadau wa Umoja Veteran ambaye pia ni kiongozi wa chuo cha IFM. Tukaongea nae pia ili tumfanye kama mlezi wetu akatukubalia ombi letu.

Nae Mzee kiongoa akajaribu kuwasiliana na kiongozi wa NIT na kwa bahati nzuri tupewa ruhusa ya kurudi tena NIT.


Inawezekana hawana uchumi wa kutosha, inawezakana baadhi ya mambo kwao yasiwe sawa. Lakini kama wakiamja kujitoa kwelikweli na TFF ikiwashikana mkono basi akademi hii itagoa matunda mazuri na mwisho tukajenga akademi nyingi zenye manufaa kwa soka letu. Kama njkvyosema La Masia sio kwamba eti walianza na mabilion ya fedha, la hasha, walianza tu kawaida ndio maana hata Messi mkataba alisaini kwenye tishu. Kila kitu kinawezekana.


Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here