Home Kimataifa Serena Williams amsambaratisha dada yake

Serena Williams amsambaratisha dada yake

7179
0
NEW YORK, UNITED STATES - SEPTEMBER 07: US OPEN 2002, New York; SIEGEREHRUNG: Venus und Siegerin Serena WILLIAMS/USA (Photo by Bongarts/Getty Images)

US Open 2018: Serena Williams amefanikiwa kufuzu hatua ya 4 baada ya kumfumua dada yake VenusSerena Williams
2018 US Open
Mahali: Flushing Meadows, New York

Ilianza tarehe: 27 August mpaka 9 Julai

Serena Williams ameafanikiwa kumuondosha dada yake Venus Williams kule New York kwenye moja ya mashindano makubwa kabisa ya Tennis duniani.

Mshindi huyo mara 23 wa Grand Slam champion, natarajia kuvunja rekodi ya Margaret Court aliyetwaa mataji 24. Serena alitumia dakika 71kabla ya kushinda kwa seti 6-1 na 6-2.

Wana ndugu hawa wenye miaka 38 na 36 walicheza mara ya 30 lakini hakuwa mchezo mgumu kiasi hicho kama wengi walivyotatajia.

Serena Williams, alipatwa na majeraha seti ya kwanza anatarajia kukutana na raia wa Estonia Kaia Kanepi kwenye hatua ya 16 bora

Kanepi mwenye miaka 33, alimbutua mshika tenis namba moja duniani Simona Halept

“Huu ulikuwa mchezo wangu bora tokea nimerud,” alisema Serena, ambaye alikuwa nje kwa sababu ya uzazi tokea mwezi wa 9 mwaka jana.

Baada ya kupoteza michezo mitatu, Serena amepata ushindibwake mkubwa dhidi ya dada tokea mwaka kule Charleston 2013.

“Sidhani kama nimecheza vibaya ila amejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wotet,” Venus aliwaambia waandishi wa habari

Serena Williams

Serena akipata matibabu

Watoto hawa wa Williams walikutakana kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya WTA Tour mwaka 1998 kwenye Australian Open.

Wotw kwa pamoja wameshinda 30 Grand Slam lakini dada yake Serena Williams amekuwa akitawala sana michuano hiyo ya wanawake

Huu ni ushindi wa 18 kwa Serena dhidi ya dada yake Venus kwenye uwanja wa Arthur Ashe Stadium.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here