Home Kitaifa Serengeti boys yaalikwa kwenye michuano nchini Uturuki

Serengeti boys yaalikwa kwenye michuano nchini Uturuki

4453
0

Baada ya Serengeti boys kutwaa Ubingwa wa COSAFA 2018 kule Botswana, Serengeti boys imepata mwaliko maalumu kushiriki kwenye mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon U17 yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki mwezi Februari 2019.

Mashindano hayo yameandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya UEFA.

Michuano hiyo itatia nanga mwezi Februari 22, 2019 na kufikia hitimisho Machi 2, 2019. Mashindano hayo yatajumuisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya.

Serengeti boys wataungana na mataifa mengine mbalimbali kutoka barani afrika kama vile Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea. Timu za Ulaya ambazo zitaungana zinafikia idadi ya timu 4.

Faida kubwa ya mashindano hayo yataipa nafasi ya Serengeti kujipima nguvu na kuoata changamoto mbalimbali ili kufanya vizuri kwenye mashindano ya AFCON 2019 ambayo yatafanyika hapa nchini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here