Home Kitaifa Serengeti Boys yafanya kweli mshindi wa tatu “U-17 CECAFA”

Serengeti Boys yafanya kweli mshindi wa tatu “U-17 CECAFA”

9492
0

Hatimaye timu ya taifa ya vijana ya umri wa miaka 17 imeshinda nafasi ya 3 kwa kuwafunga Rwanda kwa mikwaju ya penati. Hata hivyo mshambuliaji tegemezi wa Tanzania kinda Kelvin John maarufu kama “Mbappe” hakupata nafasi ya kufunga. Alionekana mara kadhaa uwanjani kucheza kwa morali ndogo huku baadhi ya watu wakidai alikuwa na huzuni sana.

Nahodha Morice alicheza soka maridhawa na kuonesha uwezo wake wa hali ya juu. Kiungo wa dimba la kati Jefferson maarufu kama Kante nae ni mmoja wa nyota waliocheza kwa kujituma sana.

Hata hivyo kitendo cha wachezaji wa Serengeti kufunga bao na kuonesha ishara ya kuomba radhi kilibeba maswali mengi. Hata hivyo mwalimu alilitolea ufafanuzi

Kauli za makocha

Kocha wa Rwanda

“Tanzania ni timu nzuri sana kuliko timu zote zilizopo hapa. Ni bahati mbaya hawajafika fainali. Mkiwasaidia watawalipa matunda mengi siku zijazo”

Kocha mkuu wa Rwanda amekisifu kikosi chs timu ya taifa ya Tanzania ya vijana.

Yeye anaamini kuwa kikosi hiki kipo imara sana. Amewaasa watanzania kuendelea kuwatia moyo wachezaji wetu ili waweze kujiimarisha zaidi.

Hata hivyo amesema kuna changamoto kadha wa kadha kwa taifa lao.

“Rwanda kupata mashindano ya watoto ni changamoto sana. Ni mara chache sana” kocha Rwanda”

Kocha mkuu wa Serengeti boys

Oscar Milambo

Amezungumzia suala la wachezaji kupewa majina ya wachezaji wakubwa kama Mbappe

“Tuwasifie wachezaji wetu kwa kiasi. Kuwaita majina ya wachezaji wakubwa sio kosa wala haiwaathiri huko ni kuwapa motisha. Mtoto akifaulu shule ukimpa zawadi haimaanisha ajilemaze ila afanye vyema zaidi ili akufurahishe”

Pia ameeleza baadhi ya changamoto za kiuchezaji kwenye kikosi chake

“Safu ya ulinzi ya Serengeti boys ilikuwa na changamoto zaidi. Mchezaji tuliyeanza nae alifeli vipimo”

Pia akaongeza kuwa baadhi ya wachezaji muhimu kukosekana kumefanya timu icheze migumo tofauti na matarajio yake.

“Tumecheza na baadhi ya wachezaji ambao hatukuwategemea. Lakini lengo letu ni kujaribu kutafuta maelewano mapya. Pia upande wa kulia ulikuwa na kasoro kadhaa na tumeona baadhi ga magoli yamepatikana kupitia upande huo.

Pia ameelezea kuwa mashindano haya yamekuja na taswira tofauti

“nimepata somo kubwa katika mashindano. Hawa watoto wapo katika maendeleo ya ukuaji lakini changamoto kubwa ni kwamba kwa bahati mbaya mashindano yamekaa kiushindani zaidi. Sio mbaya kwa sababu tunawajenga wachezaji hawa wachanga kukomaa vyema zaidi”

Kuhusu sakata la wachezaji kuomba radhi

“Wachezaji kuomba na kutokuomba radhi kwangu mimi sio jambo kubwa. Watanzania wanapaswa waangalie kile watoto wao walichokifanya. Ni kweli wale ni watoto kama walikosea wanapaswa kujituma zaidi ili kutimiza lengo”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here